Monday, 12 October 2026

DKT. KIJAJI AONGOZA KIKAO CHA KUPAMBANA NA UJANGILI WA WANYAMAPORI KIKANDA

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji ameongoza kikao cha 14 cha Baraza la Usimamizi wa Utekelezaji wa Mkataba wa Lusaka (14th Bureau of Governing Council) kilichofanyika Jijini Nairobi, nchini Kenya, kwa lengo la kuimarisha Sekretarieti ya Mkataba huo katika mapambano dhidi ya ujangili na uhalifu wa wanyamapori na misitu unaovuka mipaka ya nchi. […]

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji ameongoza kikao cha 14 cha Baraza la Usimamizi wa Utekelezaji wa Mkataba wa Lusaka (14th Bureau of Governing Council) kilichofanyika Jijini Nairobi, nchini Kenya, kwa lengo la kuimarisha Sekretarieti ya Mkataba huo katika mapambano dhidi ya ujangili na uhalifu wa wanyamapori na misitu unaovuka mipaka ya nchi.

Kikao hicho kilichowakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka zikiwemo Tanzania, Kenya, Zambia, Liberia na Republic of the Congo, kimefanyika leo Mei 20, 2026 Jijini Nairobi.

Katika kikao hicho, viongozi wamepitia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha mwaka 2025 kilichofanyika Jijini Arusha, ambapo miongoni mwa maazimio hayo ilikuwa ni kufanya maboresho ya utendaji na muundo wa Sekretarieti ya Mkataba wa Lusaka.

Aidha, kikao hicho kimejadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Sekretarieti kwa kipindi cha Mei 2025 hadi Aprili 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kukabiliana na uhalifu wa wanyamapori na misitu unaovuka mipaka kwa ufanisi zaidi.

Katika ziara hiyo, Dkt. Kijaji ameambatana na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Alexander Lobora, Mkurugenzi Msaidizi wa Kuzuia Ujangili, Ezekiel Goboro pamoja na watendaji kutoka taasisi mbalimbali za uhifadhi zikiwemo Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA), Tanzania National Parks Authority (TANAPA) na Tanzania Forest Services Agency (TFS).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *