INTER NA SAFARI YA JASHO, DAMU HADI UBINGWA SERIE A

Date:

Share post:

MILAN, Italia
MSIMU uliopita haukuwa mzuri kwa Inter Milan baada ya kuambulia patupu katika mashindano yote matatu ya ndani. Safari hii, upepo umebadilika.

Inter wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu (Serie A) walipoifunga Lazio mabao 2-0, ushindi uliowaweka kileleni kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya Napoli inayoshika nafasi ya pili.

Zikiwa zimebaki mechi tatu kwa kila timu, si Napoli wala timu yoyote ya Serie A inayoweza kufikia pointi hizo.

Timu hiyo sasa inasubiri fainali ya Kombe la Ligi, ambapo itaikabili Lazio, mchezo ukitarajiwa kuchezwa Mei 13, 2026.

Endapo Inter itashinda, basi itakuwa imemaliza msimu ikiwa na mataji makubwa mawili ya ndani, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu mwaka 2010 ikiwa chini ya kocha Jose Mourinho.

Msimu uliopita, Inter walikuwa na nafasi ya kutwaa mataji matatu (Serie A, Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa) lakini yote yaliota mbawa.

Walilikosa taji la Serie A kwa tofauti ya pointi moja nyuma ya Napoli iliyotwaa ubingwa, waliishia nusu fainali ya Kombe la Ligi, na pia walipoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kufungwa mabao 5-0 na PSG.

Katika mazingira yaliyowashitua wengi, kocha Simone Inzaghi, ambaye aliifikisha mara mbili fainali ya Ligi ya Mabingwa, alijizulu na kutimkia Al-Hilal ya Saudi Arabia.

Licha ya wengi kuponda uamuzi wa Inter kumpa ajira Cristian Chivu kwa madai ya uzoefu wake mdogo, akiiongoza Parma katika mechi 13 pekee za Serie A, ni wazi beki huyo wa zamani amewajibu kwa vitendo.

Kwa upande wao, mabingwa watetezi, Napoli, hawakuwa na upepo mzuri kwani mshambuliaji wao tegemeo, Romelu Lukaku, aliumia kabla ya msimu kuanza na kukosekana kwa miezi kadhaa.

Ni kama ilivyokuwa kwa Kevin De Bruyne, Frank Anguissa, David Neres, Billy Gilmour na Amir Rrahmani, ambao pia walikosa mechi nyingi kutokana na majeraha.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na...

WIZARA YA MAJI KUIMARISHA TEKNOLOJIA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI NCHINI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Wizara yake itaendelea kuimarisha udhibiti wa upotevu wa maji katika mifumo ya...

MAPITIO MAPYA YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA YAFANYIKA KUOANISHA NA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

Wizara ya Fedha imeanza mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo...

WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 15 KUNUFAIKA NA TEKNOLOJIA YA KAMERA ZA FUNDUS

Zaidi ya wananchi milioni 15 hadi 20 wanatarajiwa kunufaika na matumizi ya teknolojia ya Kamera za Fundus (Portable...