MANCHESTER, Uingereza
KIUNGO wa kimataifa wa Uholanzi, Tijjani Reijnders, huenda akaondoka Manchester City na kutimkia Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mwishoni mwa msimu huu.
Reijnders (27), aliwahi kuwika Serie A akiwa na kikosi cha AC Milan, kabla ya Man City kumsajili mwaka jana kwa ada ya Pauni milioni 46.3.
Baada ya kupoteza nafasi ya kuanza katika kikosi cha kocha Pep Guardiola, nyota huyo anatafuta mlango wa kutokea Etihad.
Ripoti kutoka katika vyanzo vya habari vya Italia zinaeleza kuwa saini yake inawindwa na vigogo wa Serie A, Juventus.
Kwa upande wao, Man City wako tayari kukaa mezani na klabu yoyote itakayoweka mezani ofa ya kueleweka.






