MADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid haina mpango wa kumpiga bei mshambuliaji wake wa kati raia wa Brazil, Endrick, kwa mujibu wa mtandao wa TEAMtalk.
Baada ya kushindwa kung’ara Santiago Bernabeu, Endrick amerejesha makali yake akiwa kwa mkopo Lyon ya Ligue 1.
Akiwa ameshafunga mabao saba na kutoa ‘asisti’ saba katika mechi 18 alizocheza msimu huu, Madrid imepanga kumrejesha na si kumuuza moja kwa moja.
Endrick (19), amekuwa kwenye rada za vigogo wa soka wa Kaskazini mwa Jiji la London, Arsenal na Chelsea.
Katika hatua nyingine, zipo ripoti zinazodai kuwa nyota huyo naye anavutiwa na mpango wa kubaki Madrid na kupigania namba yake kikosini.






