MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho, amesema kwa sasa akili yake iko Benfica na si Real Madrid anayohusishwa nayo.
Madrid inatajwa kumtaka Mourinho ili aiongoze timu hiyo msimu ujao. Alvaro Arbeloa ni kocha wa muda na anatarajiwa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.
Raia wa Madrid, Florentino Perez, anatajwa kuwa ni shabiki mkubwa wa Jose Mourinho na anataka kumrejesha kwenye benchi la ufundi.
Kwa upande wake, Mourinho amesema hajapokea ofa ya Madrid, zaidi ya kusikia tetesi kwenye vyombo vya habari.
“Hakuna mwakilishi wa Real Madrid niliyezungumza naye. Nawahakikishia hilo. Nimekuwa kwenye soka kwa miaka mingi, nimezoea tetesi za aina hii,” amesema.






