PETIT AITAKA CHELSEA KUMSAJILI OSIMHEN

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza
KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Emmanuel Petit, ameishauri klabu hiyo kumsajili mpachikaji mabao wa Galatasaray raia wa Nigeria, Victor Osimhen.

Chelsea imekuwa haina bahati katika usajili wa straika tangu Didier Drogba alipoondoka klabuni hapo miaka mingi iliyopita.

Hata hivyo, Petit anaamini Osimhen atamaliza mkosi uliowakumba washambuliaji wa kati wengi waliojaribu kuvaa viatu vya Drogba.

“Tangu Drogba alipoondoka, nafikiri jezi namba 9 ya Chelsea imekuwa na mkosi. Nafikiri itakuwa tofauti kwa Osimhen …” amesema Petit.

Hata hivyo, Osimhen anayesakwa pia na klabu za Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich na PSG, amesema anatamani kubaki Galatasaray kwa miaka mingi ijayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote...

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA WAKUNGA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa...

POLISI KUENDELEA KUDHIBITI WAZUSHI MITANDAONI, LIKIIMARISHA ULINZI KUELEKEA DERBY YA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya matukio mbalimbali ya kiusalama na kisheria,...

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UTENGUZI NA UHAMISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi...