RAIS ALIKATAA MESSI KURUDI BARCELONA

Date:

Share post:

CATALUNYA, Hispania

KOCHA wa zamani wa Barcelona, Xavi, amefichua kuwa alikaribia kumrejesha Lionel Messi lakini Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta, alikataa mpango huo.

Xavi anazungumzia mwaka 2023, ambapo akiwa kocha wa klabu hiyo aliiwezesha kutwaa mataji mawili kwa mpigo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Mhispania huyo amesema si Messi pekee, bali pia alijaribu kuwarudisha Neymar na Pedro.

“Nikiwa kocha wa Barcelona, nilimrejesha Dani Alves na nilijaribu kufanya hivyo pia kwa Neymar, Pedro na Messi.

“Pedro na Neymar ilishindikana kutokana na hali ngumu ya kiuchumi lakini kwa Messi ni Rais ndiye aliyekataa,” amesema.

Kwa mujibu wake, yalikuwepo mazungumzo yaliyochukua miezi mitano kati yake na Messi. “Kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri, lakini mwisho wa siku Rais alikataa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BURIANI GWIJI WA SOKA NA MAIGIZO NCHINI, HASHIM KAMBI

Tasnia ya burudani nchini Tanzania imekumbwa na majonzi kufuatia kifo cha mwigizaji na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa...

MEGAN AACHANA NA MPENZI WAKE KISA ‘KUCHEPUKA’

LOS ANGELES, Marekani BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki wa Hip hop nchini Marekani, Megan thee stallion,...

SERIKALI YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUWA MHIMILI WA UCHUMI

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026,...

KINDA AJAX AZIGONGANISHA ARSENAL, CHELSEA

LONDON, Uingereza KLABU za Arsenal na Chelsea zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya staa wa Ajax ya Uholanzi,...