Friday, 21 August 2026

KAMISHNA ALEX MKAMA AHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA POLISI NA WATENDAJI WA KATA.

Kamishna wa Polisi (CP) Alex Mkama amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa, Viongozi wa dini, Wazee wa kimila na Maafisa Usafirishaji kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia uhalifu. Hayo amezungumza katika kikao na Watendaji wa Kata na Mitaa, Viongozi wa Kimila na Maafisa Usafirishaji wa Mkoa wa Mbeya kilichofanyika Aprili 09, 2026 katika ukumbi wa […]

Kamishna wa Polisi (CP) Alex Mkama amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa, Viongozi wa dini, Wazee wa kimila na Maafisa Usafirishaji kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia uhalifu.

Hayo amezungumza katika kikao na Watendaji wa Kata na Mitaa, Viongozi wa Kimila na Maafisa Usafirishaji wa Mkoa wa Mbeya kilichofanyika Aprili 09, 2026 katika ukumbi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mbeya ambapo amewataka viongozi hao kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe mapema.

Aidha, Kamishna Mkama amekemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili katika jamii na kuwataka viongozi wa Serikali, Dini na Kimila kutofumbia macho na kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa ili kuzuia vitendo huku akisisitiza wazazi kulipa kipaumbile suala la malezi kwa watoto kuanzia ngazi ya familia.

Pia, ameitaka jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kufika Mahakamani kutoa ushahidi ili mchakato wa haki jinai uweze kukamilika na hatimaye washtakiwa waweze kutiwa hatiani kwa mujibu wa sheria.

Naye, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi Daud Dule ameahidi kuendeleza ushirikiano kati yao, Wananchi na Jeshi la Polisi na kushukuru kwa elimu iliyotolewa kwani itakuwa chachu katika kuboresha utendaji kazi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Sisimba Jijini Mbeya, Jumapili Mwasenga amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwakutanisha pamoja na kuwapa elimu itakayosaidia kuzuia uhalifu na kuimarisha na kudumisha ushirikiano kati yao na Polisi Kata.

Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP Alex Mkama ameanza ziara ya kikazi Mkoani Mbeya ambapo mbali ya kufanya vikao pia atakagua na kuangalia utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii na kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kutoa elimu, kusikiliza maoni na changamoto zinazowakabili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *