Friday, 21 August 2026

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII ZANZIBAR AFANYA ZIARA KUJIFUNZA VIKUNDI VYA MALEZI

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Anna Paul, amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayolenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu vikundi vya malezi ya watoto. Ziara hiyo inalenga kujifunza masuala ya malezi ya watoto hususan katika maeneo ya uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wa […]

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Anna Paul, amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayolenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu vikundi vya malezi ya watoto.

Ziara hiyo inalenga kujifunza masuala ya malezi ya watoto hususan katika maeneo ya uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wa Kamati za Malezi ya Watoto (Parenting Groups) katika halmashauri za Jiji la Arusha, Arusha na Meru.

Imeelezwa kuwa Programu hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la SOS Tanzania.

Katika ziara hiyo, Waziri ameambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Abeida R. Abdallah, pamoja na Mkurugenzi wa Jinsia na maafisa wengine waandamizi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *