KINSHASA, DRC
WAZIRI wa Wizara ya Michezo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Didier Bodimbo, amemtumia ujumbe mzito supastaa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo.
Bodimbo amesema timu yake ya soka ya Taifa itaifunga Ureno katika mchezo wa fainali zijazo za Kombe la Dunia na kumwacha Ronaldo akimwaga machozi.
Ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuwapongeza wachezaji wa DRC kwa kufanikisha kufuzu fainali hizo zitakazoanza Juni, 2026.
“Cristiano Ronaldo atalia atakapokutana na DR Congo” amesema Bodimbo, ambaye Taifa lake limerejea Kombe la Dunia baada ya miaka 52 ya kuikosa michuano hiyo.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, fainali za mwaka huu zitashirikisha timu 48.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha







