Monday, December 23, 2024
spot_img

HABARI PICHA – WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AKISHIRIKI KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA MIAKA 101 YA KUZALIWA KWA MWL, JULIUS NYERERE, JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye ukumbi wa Chimwaga, uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma alikokuwa mgeni rasmi katika kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mei 6, 2023. Kutoka kulia ni Naibu Spika na Mbunge wa Ilala, Azan Zungu, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Anamringi Macha, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Paul Kimiti na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 2

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Mei 6, 2023. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Anamringi Macha, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Paul Kimiti, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Naibu Spika wa Bunge, Azan Zungu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 3, 4, 5

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kongamono la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma, Mei 6, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 6, 7

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mizengo Pinda katika kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lililofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma, Mei 6, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 8, 9

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukrani Meneja Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Zawadi Kanyawana kama ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo iliyokuwa miongoni mwa wadhamini wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambalo  Waziri Mkuu Majaliwa alilihutubia kwenye ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma, Mei 6, 2023. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Paul Kimiti, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo, Mizengo Pinda, Naibu Spika wa Bunge, Azan Zungu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 10, 11

Baadhi ya washiriki wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza nao katika kongamno hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma, Mei 6, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 12

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hati ya huduma iliyotukuka, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mizengo Pinda katika kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga Jijini Dodoma, Mei 6, 2023. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Paul Kimiti. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 13

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi mche wa parachichi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sechelela ya jijini Dodoma, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Klabu za Mazingira za Mwalimu Nyerere kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu baada ya kuhutubia kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwenye ukumbi wa Chimwaga Jijini Dodoma, Mei 6, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya