Thursday, 20 August 2026

SCOTLAND FC YAIMARISHA ULINZI KWA KUWASAJILI MAKINDA WAWILI

Klabu ya Scotland FC, mabingwa watetezi wa soka nchini Zimbabwe, imetangaza rasmi kuwasajili mabeki wawili Emmanuel Jalai na Nickson Nyasulu, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kuimarisha safu yake ya ulinzi kuelekea msimu mpya wa…

Klabu ya Scotland FC, mabingwa watetezi wa soka nchini Zimbabwe, imetangaza rasmi kuwasajili mabeki wawili Emmanuel Jalai na Nickson Nyasulu, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kuimarisha safu yake ya ulinzi kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Jalai amejiunga na Scotland FC akitokea Durban City ya Afrika Kusini, klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Usajili wake unalenga kuongeza uzoefu na ubora katika eneo la ulinzi.

Nyasulu naye ametua Scotland FC akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, klabu yenye historia ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

Uzoefu wake katika soka la ndani unatarajiwa kuwa nyongeza muhimu kwa mabingwa hao watetezi.

Kupitia taarifa yake, Scotland FC imesema mabeki hao wawili ni sehemu muhimu ya mipango ya kuendelea kujenga kikosi imara, huku ikiwakaribisha na kuwatakia mafanikio katika kipindi chao kipya ndani ya klabu.

Usajili wa Jalai na Nyasulu unaonyesha dhamira ya Scotland FC ya kutetea ubingwa wake na kuendelea kuwa na ushindani mkubwa katika mashindano mbalimbali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *