Saturday, 29 August 2026

MIILI 43 YAPATIKANA BAADA YA MRIPUKO WA MGODI MYANMAR

Zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha kufuatia mripuko mkubwa uliotokea katika eneo la uchimbaji madini kaskazini mashariki mwa Myanmar, huku juhudi za uokoaji zikiendelea kutafuta manusura na miili ya wahanga wengine. Kwa mujibu wa kundi la wanamgambo la Jeshi la Ukombozi la Ta’ang (TNLA), linalodhibiti eneo hilo, watu 43 wamethibitishwa kufariki dunia kufuatia mripuko huo […]

Zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha kufuatia mripuko mkubwa uliotokea katika eneo la uchimbaji madini kaskazini mashariki mwa Myanmar, huku juhudi za uokoaji zikiendelea kutafuta manusura na miili ya wahanga wengine.

Kwa mujibu wa kundi la wanamgambo la Jeshi la Ukombozi la Ta’ang (TNLA), linalodhibiti eneo hilo, watu 43 wamethibitishwa kufariki dunia kufuatia mripuko huo uliotokea Jumapili Mei 31, 2026. Miongoni mwa waliofariki, saba ni watoto wadogo.

TNLA imesema kuwa watu wengine 112 walijeruhiwa katika tukio hilo, wakiwemo watoto 25, huku majeruhi 37 wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya. Hali hiyo imeibua hofu ya kuongezeka kwa idadi ya vifo katika siku zijazo.

Waokoaji pamoja na mashirika ya misaada wanaendelea na operesheni katika eneo hilo lenye utajiri wa madini lililopo karibu na mpaka wa Myanmar na China. Hata hivyo, juhudi hizo zimekuwa ngumu kutokana na ukubwa wa athari za mripuko huo, ambapo baadhi ya miili iliyopatikana imesambaratishwa vipande vipande.

Maeneo mengi ya uchimbaji madini nchini Myanmar yanadhibitiwa na makundi yenye silaha yanayopambana na serikali ya kijeshi ya nchi hiyo. Kutokana na mazingira hayo, matukio ya milipuko na ajali katika migodi yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kusababisha vifo pamoja na majeraha kwa wachimbaji na wakazi wa maeneo husika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *