MATUMIZI YA NISHATI SAFI YAZIDI KUSHIKA KASI WIZARA YA ULINZI

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia yameendelea kuongezeka katika taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma leo Mei 19, 2026, Dkt. Nyansaho amesema Jeshi la Kujenga Taifa limefikia asilimia 100 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na kambi zake zinazolisha zaidi ya watu 100 zimefikia asilimia 92 huku Shirika la Mzinga na Tanzania Automotive Technology Center vikifikia asilimia 98.

Aidha, amesema wizara kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea kutekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi katika kambi zote za JKT.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, hatua zilizotekelezwa ni pamoja na utengenezaji wa mashine za kuzalisha mkaa mbadala, ujenzi wa mitambo ya gesivunde pamoja na kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu utengenezaji wa mkaa banifu katika kambi za JKT.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here