Google search engine

WAARABU WAMGOMBEA MO SALAH

Share

KLABU tajiri za Ligi Kuu ya Saudi Arabia zinapigana vikumbo kuiwania huduma ya mshambuliaji anayejiandaa kuondoka Liverpool, Mohamed Salah.

Mtandao wa TEAMTalk umeripoti kuwa tayari bado ya mabosi wa klabu hizo wameshaanza kuwasiliana na wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri.

Itakumbukwa, Salah alikaribia kutua Saudia mwaka 2025, kabla ya uongozi wa Liverpool kufanikiwa kumzuia dakika za mwisho za usajili.

Safari hii, uwezekano ni mkubwa kwa nyota huyo kwenda huko baada ya kuweka wazi kuwa huu ni msimu wake wa mwisho Anfield.

Kwa sasa, klabu ya Al-Ittihad ndiyo inayohusishwa zaidi na saini yake, ingawa pia zipo za Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Uturuki.

Read more

Local News