NAIROBI, Kenya
RAIA 16 wa Kenya hawajulikani walipo baada ya kuingia Urusi na kujiunga na jeshi la nchi hiyo. Hiyo ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.
Wakati huo huo, Wizara imeeleza kuwa raia wake wengine 47 wamerejea Kenya wakitokea Ukraine walipokuwa wakiwasaidia wanajeshi wa Urusi.
Aidha, taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje imeongeza kuwa raia wengine 38 wamebaki Urusi wakiendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali.
Kwa upande mwingine, Wizara imedai kuwa inaendelea na uchunguzi ili kubaini kama raia 16 waliopotea wamefariki vitani au bado wapo hai.
Taarifa ya Wizara ilibainisha kuwa kwa sasa Kenya ina raia wake 165 walioko vitani nchini Ukraine wakiisaidia Urusi.





