Google search engine

HRW: WANAJESHI WA SERIKALI WANAUA RAIA BURKINA FASO

Share

OUAGADOUGOU, Burkina Faso

RIPOTI ya Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) imebaini kuwa wanajeshi wa Serikali ni wahusika wakuu wa mauaji ya raia nchini humo.

Burkina Faso iko chini ya utawala wa kijeshi tangu mwaka 2022 lakini bado hali ya usalama ni changamoto kubwa katika maeneo mengi nchini humo.

Kwa sasa, asilimia zaidi ya 60 ya maeneo ya Burkina Faso yako chini ya waasi, watu zaidi ya milioni 2.1 wamepoteza makazi na takribani milioni 6.5 wana uhitaji wa misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa HRW, vikosi vya jeshi la Serikali vimekuwa vikitekeleza matukio mengi ya ukatili kuliko hata vikundi vya waasi.
Aidha, ripoti ya Shirika hilo imeweka wazi kuwa watu wa jamii wa Fulani wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo.

Read more

Local News