WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Pam Bondi.
Ifahamike kuwa Bondi amekuwa mshirika mkubwa wa Rais Trump na mtetezi wa utawala wake kwa miaka mingi.
Katika taarifa yake kupitia mtandao wa kijamii wa ‘Truth Social’, Trump amemtaja Bondi kuwa ni mwanamke shupavu na kusema atampangia majukumu mengine katika sekta binafsi.
Bondi anakuwa kiongozi wa pili ‘kutumbuliwa’ na Rais Trump katika wiki za hivi karibuni baada ya Kristi Noem aliyekuwa Mkuu wa Usalama naye kung’olewa na nafasi yake kuchukuliwa na Todd Blanche.
Kwa upande wake, Bondi amesema ataendeleza bidii katika majukumu yake mapya, ingawa hakuweka wazi nafasi anayokwenda kuchukua.




