Google search engine

10 MBARONI KWA TUHUMA ZA UTAPELI

Share

RIPOTA PANORAMA

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro    linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za utapeli kwa kutumia mitandao ya simu.

Kati yao, saba wamekamatwa wakiwa na laini 110 zilizosajiliwa kwa majina ya watu tofauti katika maeneo ya Ifakara.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Alex Mkama amethibitisha watuhumiwa hao kukamatwa Machi 3, 2026 kwa nyakati tofauti baada ya oparesheni maalum iliyofanyika katika Kitongoji cha Magoha, Kata ya Lumemo wilayani humo.

Kamanda huyo amesema upelelezi unaendelea ili kuwakamata washirika zaidi wa mtandao huo na kukomesha vitendo hivyo mkoani hapa.

Read more

Local News