Arsenal waichapa PSV michuano ya Europa

0
156

bao pekee lililowekwa kimiani na Granit Xhaka katikati ya kipindi cha pili, limeiwezesha Arsenal kuendelea na moto wake wa kufanya vizuri katika michuano mbalimbali wanayoshiriki msimu huu, baada ya kuwalaza PSG Eindhoven kwa bao 1-0 kwenye pambano hilo la michuano ya Europa.

PSV inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nestelroy, waliwasili uwanja wa Emirates wakiwa katika kiwango bora kabisa kufuatia kuwa na wastani wa kufunga mabao 3 kila mechi msimu huu, lakini wakakutana na vijana wa Mikel Arteta, ambao nao wako kwenye msimu wao bora kabisa huku wakiwa wanaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza mbele ya mabingwa watetezi Man City kwa pointi nne.

Walijitahidi kuhimili mashambulizi mfululizo ya Arsenal, na kuna wakati ilionekana kama pambano hilo lingeisha kwa sare tasa ya bila kufungana, lakini Arsenal, kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika mechi nyingi msimu huu, hawakukata tamaa na juhudi zao ziliwasaidia kupata ushindi huo ambao unawafanya waongoze kundi lao huku PSV wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here