SHILOLE: natamani kupungua, tatizo msosi…

0
108
Shilole, ambaye ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mjasiriamali

MSANII wa muziki wa Bongoflava, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka sababu za kunenepa kwake kuwa ni biashara yake ya chakula anayoifanya inamfanya awe anakula mara kwa mara.

Shilole ambaye pia ni mjasiriamali, alisema kuwa alikuwa na kilo 108 lakini sasa amepunguza kilo sita na kubaki na kilo 102 huku akiweka wazi kuwa akiamka anakunywa supu asubuhi na baadaye usiku anakula wali nazi.

“Hata ungekuwa wewe jamani naamka na vyakula vizuri kwenye mgahawa wangu asubuhi supu ya kuku, ulimi bado usiku namaliza na wali nazi sina mkopo sina stress napata mapenzi mazuri kwa mwenza wangu kwanini nisinenepe,” alisema na kuongeza:

“Natamani kupungua lakini kila nikianza mazoezi nafikiria chakula ninachokula kwasababu siwezi kuacha, napenda kula kwasababu mimi muda wote nashinda na vyakula.”

Alisema kutokana na mwili wake, anashindwa kufanya mambo aliyokuwa akiyafanya miaka ya nyuma kwenye majukwaa kwa kufanya matamasha makubwa ambayo alikuwa anatumia mwili wake mdogo kucheza vizuri huku akikiri kuwa sasa bado hajaona msanii ambaye anaweza kufanya vizuri kwa kucheza kama alivyokuwa anafanya yeye wakati ule.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here