Monday, June 23, 2025
spot_img

TAKUKURU YACHUNGUZA JINAI SKENDALI YA RUSHWA YA NGONO YA BOSI WA TPA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa, Salum Hamduni


 

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeanza kuchunguza makosa ya jinai kwenye skendali ya kuomba rushwa ya ngono na kunyanyasa wanawake mahali pa kazi inayomkabili Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Gabriel Mwita Thobias.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog jana, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Hamduni alisema ameelekeza  maafisa wake kuchunguza makosa ya jinai katika skendali hiyo na kwamba uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.

Hamduni alisema uchunguzi wa skendali hiyo ulianza mwaka 2018 kwa kuchunguza makosa ya kinidhamu huku yale ya jinai yakiachwa lakini sasa kikosi kilichoundwa kitachunguza jinai kwenye skendali hiyo.

“Uchunguzi ulianza mwaka 2018 lakini wakati huo waliangalia makosa ya kinidhamu, sasa nimeelekeza uchunguzi ufanyike kuangalia jinai ndani ya suala hilo na uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Hamduni.

Machi 7, 2022, Hamduni aliiambia PANORAMA kuwa hana taarifa za kuwepo kwa faili hilo katika taasisi yake na kuahidi kufuatilia lilipo ili kujua uchunguzi ulipoishia kabla ya kuzungumza tena na PANORAMA.

“Sina taarifa za hilo faili. Acha nifuatilie kwa watu wangu nione lipo wapi na nini kiliendelea kisha nitakujulisha. Kuna mambo mawili kwenye uchunguzi, uchunguzi wa kinidhamu unaweza kumkuta mtu na hatia lakini uchunguzi wa kijinai ukamkuta hana hatia, niachie nifanye uchunguzi nitakupa taarifa,” alisema Hamduni.

Gabriel Mwita Thobias


 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipozungumzia skendali hiyo Machi 13, 2022 alisema, anasubiri uchunguzi wa vyombo vya dola ili hatua zichukuliwe.

 “Siijui historia ya ajira ya huyo Mkurugenzi, lakini ninachojua kwa afisa wa ngazi ya juu kiasi hicho mpaka kuajiriwa ni lazima kulikuwa na ‘vetting’ sasa sijui ilikuwaje.

“Kuna Tume ya uajiri na TAKUKURU na vyombo vingine vya dola acha vifanyie kazi na kama walivyosema TAKUKURU wanalisaka faili la tuhuma hizo, wakikamilisha uchunguzi watatushauri na sisi tutafanyia kazi ushauri wao.

“Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ana taratibu zake, akikamilisha uchunguzi kwa sababu ameitisha hilo faili atashauri na sisi kama Serikali tutafanyia kazi. Tunasimamia sheria,” alisema Waziri Prof. Mbarawa.

Gabriel Mwita Thobias alishtakiwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Kiwanda cha Tanzania Leaf Tobacco Company Limited (TLTC) cha  mkoani Morogoro kwa kuomba rushwa na ngono na kunyanyasa wanawake mahali pa kazi. Kabla ya kuajiriwa TPA Thobias alikuwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TLTC.  

Thobias alitiwa hatiani kwa mujibu wa taratibu za ajira kwa makosa hayo na kamati ya nidhamu iliyoundwa kuchunguza tuhuma zake ambayo kiongozi wake alikuwa mzungu, aitwaye Wayne Kluckow, ambaye anafanya kazi katika Ofisi ya Kanda ya TLTC iliyoko Afrika Kusini.

Jopo la kuchunguza na kusikiliza tuhuma za Thobias liliundwa na wajumbe vigogo walitoka nje ya nchi hasa wale wanaoshughulikia mambo ya ‘compliance’ kwa sababu ya uzito wa nafasi ya uongozi aliyokuwa nayo TLTC.

Thobias alifukuzwa kazi Oktoba 23, 2018 na nafasi yake ya Ukurugenzi wa Rasilimali Watu wa TLTC ilichukuliwa na Gladys Almas, mmoja wa wafanyakazi waliopata wakati mgumu kutoka kwake na pia aliyepata kushinikizwa na Thobias kukiuka taratibu za zabuni ili kuipata upendeleo kampuni inayotajwa kwa jina la Nice kupewa zabuni ya kulisha kiwanda cha Tumbaku.

Taarifa zinaonyesha kuwa baada ya Thobias kufukuzwa kazi, Menejimenti ya TLTC iliripoti tuhuma zake kwa TAKUKURU makao makuu ambayo ilituma timu ya maafisa uchunguzi iliyoongozwa na mtu aitwaye Hazina Mwisho iliyokwenda Morogoro kufanya uchunguzi huo.

Hata hivyo, katika hali ya sintofahamu, baadaye wachunguzi hao walikutana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Stephen Kabwe kabla ya kurejea makao makuu ambako baada ya hapo ukimya ulitawala kuhusu uchunguzi huo na zipo taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinazoonesha kuwa Dk. Kebwe ana uhusiano wa kindugu na Thobias.

 

 

 

      

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

1 COMMENT

Leave a Reply to Anonymous Cancel reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya