Katika ukitaji wake huo wa staili ya kubembeleza, sasa amekuwa gumzo kwa wana mikito kwa sababu anachokifanya ni kitu kibaya ambacho hakipaswi kufumbiwa macho bali kukemewa.
Wanaosema hivi, wanasimama kwenye hoja kwamba kijana huyu haaminiki, ni adui wa Kikwete, hampendi hata kidogo rais wetu, alikuwa akimuombea mabaya na anachokifanya sasa ni kumbembeleza ili asimtose akarudi kwenye kusaga lami, lakini kutoka moyoni hampendi hata kidogo.
Mjadala kuhusu ukitaji wa Nape ni wa muda mrefu lakini hivi karibuni umeibuka kwa nguvu baada ya kubainika kuwa anaelekea kukosa adabu hata ile ya kawaida kabisa ya kuzaliwa nayo kwa sababu ya uropokaji wake.
Wana mikito wanasema maneno yaliyojikita kwenye mwelekeo wa kumchonganisha mzee wa kukita taratibu, Joseph Warioba na mkubwa wa kaya ya wana mikito hayapaswi kuachwa hivi hivi.
Katika vijiwe vyao wana mikito siku hizi wanajadili matamshi ya Nape dhidi mzee Warioba huku wakinukuu sehemu ya alichokisema kuwa; anakerwa na lawama pamoja na lugha za dharau na kejeli za baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupitia midahalo waliyoifanya dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na mwenyekiti Kikwete.
Wakifika hapo wanasonya kwa nguvu kuashiria kuchukizwa na kudharau kauli ya Nape. Wengine wanamtukana matusi ya kwapani na wastaraabu wanasema kukosa kwake adabu hata ile ya kudunduliza na kuendekeza njaa ndiko kulikomsukuma kusema hayo aliyoyasema dhidi ya Warioba na wana mikito wenzake ili amfurahishe Kikwete.
![]() |
Jaji Warioba |
Wana mikito bwana wakikudharau huwa wana lugha ya maudhi kweli kweli! Katika vijiwe vyao wanapojadili matamshi ya Nape dhidi ya mzee Warioba, wapo wanaothubutu kusema eti ukitatange wa Nape ndiyo uliomfikisha hapo kwa sababu katika ukikitange wake huo hana tofauti na mchochezi au mtu anayewagombanisha wengine.
Katika kundi lao wajuzi wa kukita kote kote, kuna wambea ambao kazi yao ni kuvujisha siri kwa sababu kiherehere waliumbwa nacho. Hawa ndiyo wale ambao wamejivusha taarifa za uchunguzi wa awali wa wana mikito dhidi ya Nape zinazoonyesha kuwa kijana huyo ni adui namba moja wa rais Kikwete.
Kama Jakaya Kikwete atapitishwa na CCM na kuwa mgombea urais mwaka 2005 atahama nchi.
![]() |
Kikwete |
Ili kuyapa nguvu madai yao hayo, wanasema asimame Nape athubutu kukanusha kauli yake hii kama hawajatoka vifua mbele kumuumbua kwa wana mikito ili kila mpenda kukita amkite apendevyo iwe kwa mbele au hata kwa nyuma.
Kwa kiburi kilichojikita kwenye ukitaji isiopaswa kutiliwa shaka, wanasema, ambaye hasadiki haya arejee nyuma mwaka 2005 baada tu ya rais Kikwete kupitishwa kuwa mgombea urais na CCM ambapo Nape alianza kuhaha kutafuta pa kwenda na akafanikiwa kukimbilia India.
Ingawa inasemaka alikwenda kusoma lakini wana mikito hawana imani na hilo kwa sababu hata aliporejea nchini wakati Kikwete akiwa bwana mkubwa, aliingia mtaani kusaga visigino vya viatu huku akimeza mate kwa fadhila za mfanyabiashara mmoja mpaka mkubwa wa kaya Kikwete alipomuonea huruma na kumpa kaukumbwa katika ufalme wake.
Wakiwa katika mshangao wao huo, wanaendelea kumchimba wakiangalia sababu ya kufurushwa kwenye umoja wa vijana wa chama cha wana mikitona kukimbilia chama cha upinzani; na sasa wakisubiri afanye kosa la kujikita kwenye uropokaji wake dhidi yao ili wapate kumkita kwa mikito ya nguvu inayotikisa kote kote.