{"id":9956,"date":"2026-04-27T09:07:58","date_gmt":"2026-04-27T09:07:58","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9956"},"modified":"2026-04-27T09:08:04","modified_gmt":"2026-04-27T09:08:04","slug":"vita-vinavyoiumiza-sekta-ya-afya-nchini-sudan","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9956","title":{"rendered":"VITA VINAVYOIUMIZA SEKTA YA AFYA NCHINI SUDAN"},"content":{"rendered":"\n<p>DARFUR, Sudan<br>IKIWA ni miaka mitatu sasa tangu Sudan ilipoingia kwenye machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, sekta ya afya nchini humo inapitia wakati mgumu zaidi.<\/p>\n\n\n\n<p>Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) linaeleza kuwa watu milioni 34 wanahitaji msaada, huku milioni 21 wakikosa huduma za afya kutokana na vita hivyo.<\/p>\n\n\n\n<p>WHO inaeleza pia, visa vya magonjwa ya mlipuko na utapiamlo vimeongezeka zaidi katika maeneo mengi ya Taifa hilo.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Vita nchini Sudan vimehatarisha maisha na vimewanyima watu haki zao za msingi, zikiwamo za afya, maji, chakula na usalama.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Mifumo ya afya imeanguka na kuacha mamilioni ya watu wakikosa huduma za afya,&#8221; amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Madaktari na wahudumu wengine wa afya wanaweza kuokoa maisha lakini wanahitaji sehemu salama za kufanya kazi ili kufikiwa na dawa za kutoa huduma.&#8221;<\/p>\n\n\n\n<p>Katika ripoti yake ya mwaka 2026, WHO inaeleza kuwa watu zaidi ya milioni 4 nchini Sudan wanasumbuliwa na utapiamlo.<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati huo huo, magonjwa kama Malaria, Dengue na Polio yameonekana kukita mizizi katika maeneo mengi, hasa Al Jazirah, Darfur, Gedaref, Khartoum na Kordofan.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Katika majimbo 18 ya Sudan, asilimia 37 ya vituo vya afya havifanyi kazi. Vifaa, magari ya wagonjwa, wagonjwa na wahudumu wa afya wamekuwa wakishambuliwa,&#8221; imeeleza ripoti hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Inaongeza kuwa yamefanyika mashambulizi 217 kwenye eneo la afya tangu mwaka 2023 na kusababisha vifo 2052 na majeruhi 810.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Mfano mzuri ni shambulizi la hivi karibuni katika Hospitali ya El Daein lililosababisha vifo 64, wakiwamo watoto na wahudumu wa afya,&#8221; imeeleza ripoti ya WHO.<\/p>\n\n\n\n<p>Je, WHO imefanya nini katika kuokoa sekta ya afya nchini Sudan? Dkt. Shible Sahbani, ambaye ni Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Sudan, amesema:<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cWHO imekuwa hapa (Sudan) tangu vita vilipoanza, ikisambaza vifaa-tiba, kufuatilia hali ya magonjwa, kuendesha na kuratibu mafunzo.&#8221;<\/p>\n\n\n\n<p>Tangu Aprili, 2023, WHO imechangia tani za ujazo zaidi ya 3300 za dawa mbalimbali, zikiwamo za magonjwa ya Kipindupindu na Malaria.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia, WHO imesaidia tiba kwa watoto zaidi ya 118,000 waliokuwa kwenye hali mbaya kutokana na utapiamlo. Chanjo za magonjwa mbalimbali zimewafikia watu zaidi ya milioni 46.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>DARFUR, SudanIKIWA ni miaka mitatu sasa tangu Sudan ilipoingia kwenye machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, sekta ya afya nchini humo inapitia wakati mgumu zaidi. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) linaeleza kuwa watu milioni 34 wanahitaji msaada, huku milioni 21 wakikosa huduma za afya kutokana na vita hivyo. WHO inaeleza pia, [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9957,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[81],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9956","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-makala-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/2f2f7974-3dd8-46ab-ab93-385e56ae26d0.jpeg?fit=463%2C279&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9956","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9956"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9956\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9958,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9956\/revisions\/9958"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9957"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9956"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9956"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9956"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9956"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}