{"id":9797,"date":"2026-04-21T06:53:52","date_gmt":"2026-04-21T06:53:52","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9797"},"modified":"2026-04-22T06:57:38","modified_gmt":"2026-04-22T06:57:38","slug":"nini-chanzo-cha-bifu-zito-la-mapacha-wa-p-square","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9797","title":{"rendered":"NINI CHANZO CHA &#8216;BIFU&#8217; ZITO LA MAPACHA WA P-SQUARE?"},"content":{"rendered":"\n<p>LAGOS, Nigeria<\/p>\n\n\n\n<p>MAMBO yamezidi kuwa mabaya kwa mapacha waliowahi kutikisa soko la muziki barani Afrika kupitia Kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye.<\/p>\n\n\n\n<p>Okoye ametangaza rasmi kubadili tarehe yake ya kuzaliwa ili asiwe anachangia &#8216;birthday&#8217; na ndugu yake, Paul.<\/p>\n\n\n\n<p>Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, amesema kwa sasa birthday yake haitakuwa Novemba 18 kama zamani.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cNatangaza rasmi. Novemba 18 siyo tena tarehe yangu ya kuzaliwa. Ifahamike kuwa sitopokea meseji za pongezi wala zawadi katika siku hiyo,&#8221; amesema na kudokeza kuwa birthday yake itakuwa Novemba 30.<\/p>\n\n\n\n<p>Hatua hiyo ni mwendelezo wa uadui mkubwa uliopo kati ya mapacha hao. Mwaka 2025, Peter alitangaza kuwa kwa sasa hataki ukaribu na familia yao yote.<\/p>\n\n\n\n<p>Je, zipi sababu za mapacha hao kuwa &#8216;chui na paka&#8217;? Makala haya yanachambua, yakianzia historia ya Kundi la P-Square.<\/p>\n\n\n\n<p>Peter na Paul walianzisha P-Square mwaka 2003. Ni kundi lililopata umaarufu mkubwa si tu Nigeria, bali pia ndani na nje ya Afrika.<\/p>\n\n\n\n<p>Miaka miwili baadaye, waliingiza sokoni albamu yao ya kwanza, &#8216;Get Squared&#8217;, iliyokuwa na ngoma kali, ikiwamo &#8216;Bizzy Body&#8217;.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 2015, wakiwa tayari ni wasanii wakubwa na wenye mafanikio, ikiwamo albamu yao kali ya &#8216;The Invasion&#8217;, ilianza kusikika minong&#8217;ono juu ya uhusiano wao kutikisika.<\/p>\n\n\n\n<p>Nyuma ya pazia, zilitajwa sababu mbalimbali zilizosababisha mgogoro. Miongoni mwanzo ni masuala ya fedha.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 2017, jipu lilipasuka rasmi baada ya wawili hao kutangaza kuvunjika kwa Kundi la P-Square. Peter ndiye aliyetangaza kujitoa kwa madai ya kutokuwapo na maelewano kati yake, Paul na uongozi (kaka yao aitwaye Jude).<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati mambo yakiwa hivyo, ilivuja video ikiwaonesha Paul na Peter wakikaribia kurushiana makonde mbele ya mwanasheria.<\/p>\n\n\n\n<p>Baadaye, waliuza nyumba waliyokuwa wakimiliki pamoja kama P-Square na kila mmoja akapata mgawo wake na kuendelea na maisha.<\/p>\n\n\n\n<p>Peter alianza kujiita &#8216;Mr. P&#8217;, wakati Paul ambaye inaelezwa kuwa bado anaungwa mkono na kaka yao, Jude, aliona ajiite &#8216;Rudeboy&#8217;.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 2021, walionekana mara kadhaa wakifanya shoo pamoja, kabla ya kurejesha Kundi lao la P-Square na kuachia ngoma kadhaa, zikiwamo &#8216;Jaiye&#8217; na &#8216;Find Somebody&#8217;.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, mwaka 2024 wawili hao walitemana tena. Kwa mujibu wa Paul, Peter alimtumia meseji akimwambia havutiwi kuendelea kufanya naye kazi.<\/p>\n\n\n\n<p>Paul hakuishia hapo. Alisema Peter &#8216;alimchoma&#8217; yeye na kaka yao, Jude, kwa Taasisi ya Uhalifu wa Kiuchumi (EFCC) kwa madai ya utakatishaji fedha.<\/p>\n\n\n\n<p>Kama itakumbukwa, Paul aliitwa na kuhojiwa na EFCC, kabla ya kuachiwa baada ya kukutwa hana hatia.<\/p>\n\n\n\n<p>Mbali ya masuala ya fedha, zipo sababu zingine zinazotajwa kuchangia &#8216;damu mbaya&#8217; kati ya Peter na Paul.<\/p>\n\n\n\n<p>Peter amewahi kusema alichukuliwa kama mfanyakazi katika Kundi na si sehemu ya wamiliki. Kutokana na hilo, aliomba kaka yao, Jude, asiendelee kuwa meneja, jambo ambalo hakusikilizwa.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia, kuna suala la familia. Zipo taarifa kuwa Peter hakuwa akifurahia namna mkewe, Lola Omotayo, alivyokuwa akipuuzwa na kaka yao, Jude, na ndugu wengine wa familia yake.<\/p>\n\n\n\n<p>Vilevile, kitendo cha mashabiki kujenga mijadala ya nani mkali kati ya Paul na Peter kilitengeneza wivu na chuki kati ya wawili hao, hivyo kuliangusha Kundi hilo.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LAGOS, Nigeria MAMBO yamezidi kuwa mabaya kwa mapacha waliowahi kutikisa soko la muziki barani Afrika kupitia Kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye. Okoye ametangaza rasmi kubadili tarehe yake ya kuzaliwa ili asiwe anachangia &#8216;birthday&#8217; na ndugu yake, Paul. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, amesema kwa sasa birthday yake haitakuwa Novemba [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9798,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[88],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9797","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-burudani"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/486188f0-68a3-4bc5-b17b-86381f844e1e.jpeg?fit=588%2C330&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9797","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9797"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9797\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9799,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9797\/revisions\/9799"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9798"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9797"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9797"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9797"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9797"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}