{"id":9783,"date":"2026-04-19T14:02:36","date_gmt":"2026-04-19T14:02:36","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9783"},"modified":"2026-04-19T14:02:42","modified_gmt":"2026-04-19T14:02:42","slug":"soma-hiyo-israel-ndiyo-waasisi-wa-mikwaju-ya-penalti","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9783","title":{"rendered":"SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI"},"content":{"rendered":"\n<p>LONDON, Uingereza<\/p>\n\n\n\n<p>NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini dhidi ya Hull City na dakika za nyongeza za mchezo huo wa michuano maalumu ya &#8216;pre-season&#8217; zinamalizika kwa sare ya bao 1-1.<\/p>\n\n\n\n<p>George Best wa Man United akawa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kupiga penalti tangu ilipotangaza kuwa mikwaju ya penalti itatumika kuamua mshindi katika hatua ya mtoano.<\/p>\n\n\n\n<p>Hiyo ikawa ni mara ya kwanza katika historia ya soka kushuhudia mshindi wa mechi za mtoano akipatikana kwa mikwaju ya penalti baada ya sare. Man United ilishinda.<\/p>\n\n\n\n<p>Historia inaonesha kuwa kabla ya ujio wa penalti, mshindi wa hatua ya mtoano katika mechi iliyomalizika kwa sare aliamuliwa kwa timu hizo kurudiana, kurusha sarafu, kuchagua karatasi, au idadi ya kona.<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati wa fainali za Euro mwaka 1968, Italia iliingia fainali kwa njia ya kurusha sarafu baada ya suluhu dhidi ya Umoja wa Soviet katika mchezo wa nusu fainali.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika mechi ya fainali, Italia na Yugoslavia zilitoka sare ya bao 1-1 na bingwa (Italia) alipatikana katika mchezo wa marudiano kwa ushindi wa mabao 2-0.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 1968, wakati wa michuano ya Olimpiki, timu ya soka ya taifa ya Israel ilitoka sare ya bao 1-1 na Bulgaria katika mchezo wa fainali.<\/p>\n\n\n\n<p>Ili kupata bingwa, mwamuzi alisimamia zoezi la kila nahodha kuchagua karatasi moja kati ya nyingi zilizokuwa kwenye kofia.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika karatasi hizo, ndani yake kulikuwa na ujumbe wa aidha &#8216;No&#8217; au &#8216;Yes&#8217;. Nahodha wa Israel alichagua katarasi yenye No, ikimaanisha kuwa &#8216;amekataa&#8217; ubingwa. Bulgaria wakatwaa taji.<\/p>\n\n\n\n<p>Kitendo hicho kiliuma kiongozi wa Chama cha Soka nchini Israel, Yosef Dagan, hivyo kwa kushirikiana na mwenzake, Michael Almog, waliliandikia barua Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwaka 1969 wakipendekeza mikwaju ya penalti iamue mshindi katika mazingira ya aina hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Kama ambavyo imekuwa ikifanyika hadi leo, walipndekeza wachezaji watano wa kila timu waanze kupiga penalti na kama bado timu hizo zitakuwa sare, basi waendelee kupiga wengine hadi mmoja atakapokosa na mwenzake akapata.<\/p>\n\n\n\n<p>Licha ya kuzua mjadala mkubwa, FIFA na Bodi ya Chama cha Soka cha Kimataifa (Ifab) zilipitisha pendekezo hilo rasmi Juni 27, 1970.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini dhidi ya Hull City na dakika za nyongeza za mchezo huo wa michuano maalumu ya &#8216;pre-season&#8217; zinamalizika kwa sare ya bao 1-1. George Best wa Man United akawa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kupiga [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9784,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[215],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9783","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/28ef4538-098a-45a8-852a-32870a85c15f.jpeg?fit=594%2C335&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9783","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9783"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9783\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9785,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9783\/revisions\/9785"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9784"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9783"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9783"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9783"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9783"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}