{"id":9780,"date":"2026-04-19T14:01:11","date_gmt":"2026-04-19T14:01:11","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9780"},"modified":"2026-04-19T14:01:19","modified_gmt":"2026-04-19T14:01:19","slug":"amejipata-lampard-alivyorejea-epl-akiweka-rekodi","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9780","title":{"rendered":"AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI"},"content":{"rendered":"\n<p>LONDON, Uingereza<\/p>\n\n\n\n<p>IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea Ligi Kuu ya England (EPL).<\/p>\n\n\n\n<p>Lampard aliyewahi kucheza na kuinoa Chelsea, anakuwa kocha pekee kuirudisha EPL tangu Coventry iliposhuka miaka 25 iliyopita.<\/p>\n\n\n\n<p>Timu hiyo imekata tiketi ya kucheza EPL msimu ujao (2026-27) baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Blackburn, huku wakiwa na mechi tatu mkononi.<\/p>\n\n\n\n<p>ANGUKO LAKE EPL<\/p>\n\n\n\n<p>Aliwahi kuinoa Everton kwa miezi 12 lakini aliishia kufukuzwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata alipokabidhiwa Chelsea, bado hali ilikuwa mbaya kwa upande wake. Alitimuliwa akiwa ameshinda mechi moja tu kati ya 11 alizokaa kwenye benchi la ufundi.<\/p>\n\n\n\n<p>HAIKUWA RAHISI<\/p>\n\n\n\n<p>Coventry ilimpa ajira miezi 18 iliyopita, akichukua nafasi ya kocha Mark Robins aliyekuwa ameitoa timu hiyo League Two (Daraja la Pili) hadi Championship (Daraja la Kwanza).<\/p>\n\n\n\n<p>Aliikuta timu hiyo ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Championship na msimu wa 2024-25 uliisha wakiwa wameshindwa kupanda Daraja baada ya kufungwa na Sunderland katika nusu fainali ya Sunderland.<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati wa dirisha kubwa, Lampard alifanya usajili wa kuboresha kikosi kwa kuwanasa Kaine Kesler-Hayden (Aston Villa), Luke Woolfenden (Ipswich) na Carl Rushworth (Brighton).<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati huo pia, alifanikiwa kuwabakiza wachezaji muhimu, wakiwamo Bobby Thomas na Milan van Ewijk aliyekuwa kwenye rada za Wolfsburg ya Bundesliga.<\/p>\n\n\n\n<p>Chini ya Lampard, mshambuliaji Jack Rudoni amekuwa moto wa kuotea mbali, akifunga mabao 15 katika mechi 17 alizocheza akiwa na kocha huyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Ni kutokana na mikakati mizuri kwenye usajili, sambamba na mbinu zake uwanjani, Coventry imeshinda mechi 42 kati ya 79 ilizocheza chini ya Lampard aliyeajiriwa Novemba, 2024.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea Ligi Kuu ya England (EPL). Lampard aliyewahi kucheza na kuinoa Chelsea, anakuwa kocha pekee kuirudisha EPL tangu Coventry iliposhuka miaka 25 iliyopita. Timu hiyo imekata tiketi ya kucheza EPL msimu ujao (2026-27) baada ya sare ya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9781,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[215],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9780","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/6553a19e-bf6a-4f02-8112-96351ba76ca7.jpeg?fit=739%2C415&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9780","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9780"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9780\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9782,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9780\/revisions\/9782"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9781"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9780"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9780"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9780"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9780"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}