{"id":9774,"date":"2026-04-18T10:09:11","date_gmt":"2026-04-18T10:09:11","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9774"},"modified":"2026-04-18T10:09:18","modified_gmt":"2026-04-18T10:09:18","slug":"kifo-cha-bosi-kinavyoitesa-leicester-city","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9774","title":{"rendered":"KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY"},"content":{"rendered":"\n<p>LONDON, Uingereza<br>MIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya vigogo Manchester United, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester City.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa sasa, Leicester iko hoi na inakaribia kuangukia Ligi Daraja la Pili ya England (League One) kutokana na mwenendo wake mbaya msimu huu wa Championship (Daraja la Kwanza). Nini shida?<\/p>\n\n\n\n<p>Tatizo lilianzia pale alipofariki aliyekuwa mmiliki wa klabu hiyo, Vichai Srivaddhanaprabha. Bilionea huyo alipoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea nje ya uwanja wao mwaka 2018.<\/p>\n\n\n\n<p>Srivaddhanaprabha raia wa Thailand ndiye aliyekuwa akisuka na kusimamia mikakati ya klabu, ikiwamo usajili wa wachezaji.<\/p>\n\n\n\n<p>Tangu kuondoka kwake kwenye uso wa dunia, ni kama Leicester City imekosa uongozi thabiti, licha ya kwamba klabu hiyo imekuwa ikitumia fedha nyingi kusajili wachezaji.<\/p>\n\n\n\n<p>Endapo Srivaddhanaprabha angekuwepo, huenda asingekubali straika wao tegemeo, Jamie Vardy, kuondoka klabuni hapo.<\/p>\n\n\n\n<p>Unamzungumzia mchezaji ambaye amefunga mabao 198 katika miaka 13 aliyoitumikia timu hiyo. Mchezaji ambaye amekuwa &#8216;roho&#8217; ya timu kwa muda wote huo, ikiwamo wakati wa ubingwa wa Ligi mwaka 2016.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia, tangu Srivaddhanaprabha alipofariki, Leicester City imeshuhudiwa ikiwa &#8216;jehanamu&#8217; kwa makocha. Tangu alipofukuzwa Brendan Rodgers mwaka 2023, timu hiyo imeshanolewa na watano (Dean Smith, Enzo Maresca, Steve Cooper, Ruud van Nistelrooy na Marti Cifuentes).<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa sasa, kikosi kipo chini ya Gary Rowett, ambaye miaka miwili iliyopita aliiongoza Birmingham kushuka daraja.<\/p>\n\n\n\n<p>Kuondoka kwa skauti Steve Walsh, ambaye ndiye aliyeibua vipaji vya Vardy, N\u2019Golo Kante na Riyad Mahrez nako kuliacha maswali.<\/p>\n\n\n\n<p>Kukosekana kwa uongozi imara kama wa Srivaddhanaprabha kumeifanya Leicester City kuwa klabu inayoangukia kwenye hasara kwa upande wa biashara.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 2025, klabu hiyo iliingiza hasara ya Pauni milioni 71. Kwa miaka mitatu ya hivi karibuni, hasara imefikia Pauni milioni 180.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya vigogo Manchester United, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester City. Kwa sasa, Leicester iko hoi na inakaribia kuangukia Ligi Daraja la Pili ya England (League One) kutokana na mwenendo wake mbaya msimu huu wa Championship (Daraja la Kwanza). [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9775,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[215],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9774","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/d80c696f-9127-4567-a492-0bf7c25b421c.jpeg?fit=466%2C659&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9774","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9774"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9774\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9776,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9774\/revisions\/9776"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9775"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9774"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9774"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9774"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9774"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}