{"id":9750,"date":"2026-04-17T15:19:57","date_gmt":"2026-04-17T15:19:57","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9750"},"modified":"2026-04-17T15:20:04","modified_gmt":"2026-04-17T15:20:04","slug":"marekani-cuba-mzozo-mwingine-unaosubiri-kuitikisa-dunia","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9750","title":{"rendered":"MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA"},"content":{"rendered":"\n<p>HAVANA, Cuba<br>RAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.<\/p>\n\n\n\n<p>Rais Trump amenukuliwa mara kadhaa akitishia kuivamia Cuba, akisema ana uwezo wa kufanya chochote katika Kisiwa hicho.<\/p>\n\n\n\n<p>Diaz-Canel amesema Cuba itafanya kila namna, ikiwamo kuingia vitani na kusaka ushindi, ikiwa Marekani itajaribu kuivamia.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Hatutaki ugomvi lakini ni jukumu letu kujiandaa kuepeuka. Na kama itashindikana (kuzuia vita), basi tushinde,&#8221; amesema Rais huyo.<\/p>\n\n\n\n<p>HISTORIA YA MGOGORO<br>Mataifa hayo jirani yamekuwa na uhasama mkubwa tangu mwaka 1959 baada ya Marekani kutokuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yalimuingiza madarakani Fidel Castro.<\/p>\n\n\n\n<p>Historia inakumbusha, Castro aliingia Ikulu kwa kuipindua Serikali ya Rais Fulgencio Batista iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 1961, Marekani ilijaribu bila mafanikio kuivamia Cuba baada ya Rais Castro kubinafsisha mali na biashara zote zilizokuwa zikimilikiwa na Taifa hilo nchini mwake.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika kujibu mapigo, Rais wa Marekani wakati huo, John F. Kennedy, iliweka zuio la kupeleka bidhaa zake Cuba, pia kutoingiza sukari kutoka kwa majirani zao hao.<\/p>\n\n\n\n<p>TRUMP NA NJIA YAKE TOFAUTI<br>Ikiwa ni miaka mingi imepita tangu mvutano huo kutokea, utawala wa Rais Trump, hasa awamu yake ya pili madarakani, umeonekana kuuongezea kasi uhusiano mbaya uliopo kati ya mataifa hayo.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, wanauona uongozi wa Rais Trump ukiwa umerejesha nyuma hatua kubwa iliyokuwa imepigwa na watangulizi wake (Barack Obama na Joe Biden) katika kujenga mahusiano kati ya mataifa hayo.<\/p>\n\n\n\n<p>Obama alifanya mazungumzo kadhaa na Rais wa Cuba wakati huo, Raul Castro, na mafanikio yake yakawa ni nchi hizo kuanza kushirikiana katika nyanja za kidiplomasia na biashara.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Biden naye alipiga hatua nyingine kubwa, akilegeza baadhi ya vikwazo vya Marekani kwa Cuba.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika utawala wake, Rais Trump amerejesha na hata kuzidisha vikwazo vya kusafiri na kiuchumi kwa Cuba, akiitaja Serikali ya nchi hiyo kufadhili ugaidi.<\/p>\n\n\n\n<p>Kama hiyo haitoshi, amekiwa akiitaja mara kadhaa Cuba kuwa ni tishio kwa Marekani kutokana na uhusiano wake na &#8216;maadui&#8217; zake, ikiwamo Urusi.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika kuhakikisha anaibana pumzi zaidi, utawala wa Rais Trump umezuia takribani meli zote za mafuta zinazoingia Cuba.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, ameziwekea tozo ya bidhaa zinazoingia Marekani nchi zote zinazofanya biashara ya mafuta na nchi hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Hiyo imechagiza kwa kiasi kikubwa Cuba kukosa umeme wa uhakika, kupanda kwa gharama za vyakula, huku sekta ya afya nayo ikitajwa kuwa taabani.<\/p>\n\n\n\n<p>CUBA KAMA VENEZUELA?<br>Mwaka 2025, aliagiza meli za Marekani kuzamisha baharini boti za Cuba alizodai kuwa zimebeba dawa za kulevya.<\/p>\n\n\n\n<p>Ni kama alivyoifanya Venezuela, kabla ya kuagiza wanajeshi wake kuingia nchini humo na kumng&#8217;oa madarakani Rais wa wakati huo, Nicolas Maduro.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata baada ya Maduro kukamatwa, Rais Trump aliweka wazi azima yake ya kuhamishia nguvu Cuba, ingawa baadaye Marekani iliigeukia Iran na kuanza kuishambulia Februari 28, 2026.<\/p>\n\n\n\n<p>Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaiona dhamira ya Marekani ya kuing&#8217;oa Serikali iliyoko madarakani, kama ilivyotokea Venezuela.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais wa Marekani, Donald Trump. Rais Trump amenukuliwa mara kadhaa akitishia kuivamia Cuba, akisema ana uwezo wa kufanya chochote katika Kisiwa hicho. Diaz-Canel amesema Cuba itafanya kila namna, ikiwamo kuingia vitani na kusaka ushindi, ikiwa Marekani itajaribu kuivamia. [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9751,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[81],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9750","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-makala-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/marekani.jpeg?fit=588%2C393&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9750","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9750"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9750\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9752,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9750\/revisions\/9752"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9751"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9750"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9750"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9750"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9750"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}