{"id":9735,"date":"2026-04-17T10:51:51","date_gmt":"2026-04-17T10:51:51","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9735"},"modified":"2026-04-17T10:51:53","modified_gmt":"2026-04-17T10:51:53","slug":"viongozi-longido-watakiwa-kuharakisha-uanzishaji-wa-juhizina","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9735","title":{"rendered":"VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA"},"content":{"rendered":"\n<p>Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ziwa Natron (JUHIZINA) ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Jumuiya hiyo inatarajiwa kuhudumia tarafa tatu ambazo ni Longido, Engarenaibor na Kimokouwa, kwa lengo la kuboresha usimamizi wa rasilimali za wanyamapori na kuongeza fursa za maendeleo kwa jamii zinazozunguka eneo hilo.<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumza katika kikao maalum cha kujadili maendeleo ya uanzishwaji wa JUHIZINA kilichofanyika katika Ukumbi wa J.K. Nyerere, Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Thomas Ngobei, alisema ni muhimu viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ipasavyo ili kufanikisha swala Hilo.<\/p>\n\n\n\n<p>Mhe. Ngobei alisisitiza kuwa, kwa kushirikiana na madiwani, ataweka msukumo mkubwa kuhakikisha mchakato huo unakamilika kabla ya kumalizika kwa kipindi chake cha uongozi.<\/p>\n\n\n\n<p>Alifafanua kuwa changamoto zilizokuwepo awali, ikiwemo migogoro midogo katika baadhi ya vijiji, tayari zimetatuliwa na hivyo hakuna kikwazo kinachoweza kuchelewesha uanzishwaji wa jumuiya hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cKwa sasa hakuna kijiji hata kimoja kinachopinga kuundwa kwa JUHIZINA. Nitasimamia kikamilifu kuhakikisha mchakato huu unakamilika,\u201d alisisitiza Mhe. Ngobei.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, alieleza kuwa Kamati Maalum ya Ufuatiliaji wa mchakato huo inaendelea na kazi zake, na kwamba itafanya kikao na kamati iliyoundwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ili kujadili namna bora ya kukamilisha hatua zilizobaki.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande mwingine, Mwenyekiti huyo aliwataka wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa kamati hiyo pindi itakapofika katika maeneo yao, ili kuwezesha ukusanyaji wa taarifa muhimu zitakazosaidia kukamilisha uanzishwaji wa JUHIZINA kwa ufanisi.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ziwa Natron (JUHIZINA) ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi. Jumuiya hiyo inatarajiwa kuhudumia tarafa tatu ambazo ni Longido, Engarenaibor na Kimokouwa, kwa lengo la kuboresha usimamizi wa rasilimali [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":12,"featured_media":9736,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[255],"class_list":{"0":"post-9735","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/5a138104-4623-4798-8090-3fcb75104816.jpeg?fit=720%2C476&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9735","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/12"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9735"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9735\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9737,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9735\/revisions\/9737"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9736"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9735"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9735"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9735"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9735"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}