{"id":9695,"date":"2026-04-14T14:40:29","date_gmt":"2026-04-14T14:40:29","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9695"},"modified":"2026-04-16T14:44:25","modified_gmt":"2026-04-16T14:44:25","slug":"makonda-na-kofia-ya-unabii-sekta-ya-michezo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9695","title":{"rendered":"MAKONDA NA \u201cKOFIA YA UNABII\u201d SEKTA YA MICHEZO"},"content":{"rendered":"\n<h3 class=\"wp-block-heading\">WAUMINI wa dini mbili kubwa nchini, Uislam na Ukristo, wanaweza kukubaliana kwa urahisi kwamba manabii (mitume) walitumwa katika jamii zilizokuwa zimezama kwenye maovu na kupoteza mwelekeo wa maisha. Kusudio lao halikuwa tu kuhimiza ibada sahihi, bali kurekebisha mwenendo wa jamii kwa ujumla, kuijenga kimaadili, kiuchumi na kijamii.<\/h3>\n\n\n\n<p>Katika simulizi za Qur\u2019an na Biblia, tunakumbushwa mfano wa Nabii Musa ambaye alikuta jamii ya Wamisri ikiwa imeoza: kuabudu sanamu, kushamiri kwa ushirikina, ulevi na hata kamari. Kwa ufupi, dhamira ya Mungu kwake ilikuwa ni kuibadili jamii hiyo na kuirejesha katika njia iliyo sahihi na yenye manufaa.<\/p>\n\n\n\n<p>Taswira hiyo ndiyo inanifanya nimtazame Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, katika nafasi yake ya sasa. Na hapa ninamaanisha kwa uzito wote: ameingia kwenye sekta yenye changamoto nyingi, inayohitaji \u201cmtu wa mabadiliko.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Ukweli usiohitaji mjadala mrefu ni kwamba sekta ya michezo imekuwa mhimili muhimu wa maendeleo nchini. Mbali na kodi zinazolipwa na klabu, vyama na mashirikisho, michezo pia imekuwa ikipunguza mzigo wa ajira kwa Serikali kwa kutoa fursa kwa vijana wengi kujiajiri na kuajiriwa.<\/p>\n\n\n\n<p>Zaidi ya hapo, michezo imekuwa na mchango mkubwa katika kuinua sekta nyingine, hususan utalii. Kupitia mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, klabu kutoka mataifa mbalimbali zimekuwa zikija nchini na kuleta \u201culaji\u201d kwa hoteli, usafiri na biashara za ndani.<\/p>\n\n\n\n<p>Na sasa, Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kwa kushirikiana na majirani Kenya na Uganda, hakuna shaka kuwa utalii na uchumi kwa ujumla vinatarajiwa kufaidika zaidi.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, pamoja na faida zote hizo, sekta ya michezo imeendelea kubeba mzigo mkubwa wa migogoro, inayochangiwa zaidi na udhaifu wa uongozi. Kwa miaka mingi, migogoro imekuwa kama sehemu ya maisha ya kawaida ndani ya vyama na mashirikisho.<\/p>\n\n\n\n<p>Vyanzo vyake vimekuwa vikijirudia: viongozi kung\u2019ang\u2019ania madaraka, \u201cfigisu\u201d za uchaguzi, ukosefu wa uwazi wa mapato na matumizi, pamoja na malalamiko ya mifumo kandamizi isiyotoa haki kwa wanachama na wadau.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mazingira hayo, ni wazi kabisa Waziri Makonda amepewa wizara yenye \u201cmoto\u201d\u2014sekta yenye hitaji kubwa la kusafishwa na kurekebishwa, kama ambavyo manabii walitumwa kwenye jamii zilizojaa uovu.<\/p>\n\n\n\n<p>Lakini kwa bahati nzuri, hatua chache alizochukua tangu ateuliwe zimeanza kuibua matumaini mapya na kurejesha tabasamu kwa wadau wa michezo waliokuwa wameanza kukata tamaa.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika mkutano wake na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na viongozi wa vyama na mashirikisho uliofanyika Machi 13, 2026, Waziri Makonda aligusa maeneo nyeti kwa ujasiri, akionyesha uelewa mpana wa matatizo yaliyopo na kuweka wazi njia anazotaka kuzitumia kuyatatua.<\/p>\n\n\n\n<p>Alisema: <em>\u201cViongozi wote wa vyama na mashirikisho ya michezo ambao hawajatekeleza ahadi walizotoa wakati wa kuomba uongozi nitawafuatilia. Nikibaini kuwa uongozi haujafikia hata asilimia 20 ya malengo, nitawaondoa bila huruma, kwa kuwa nafasi hizo zimepatikana kwa kura za wanachama.\u201d<\/em><\/p>\n\n\n\n<p>Kauli hii inaonyesha dhamira ya kuijenga sekta ya michezo katika msingi wa uwajibikaji\u2014utamaduni ambao kwa muda mrefu umekuwa ukikosekana kwa baadhi ya viongozi.<\/p>\n\n\n\n<p>Hatua yake nyingine iliyoibua gumzo kubwa ni uamuzi wa kuusimamisha uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufuatia malalamiko ya baadhi ya wagombea. Hili limeonekana kama ishara ya wazi kuwa hataki kuona michakato ya uchaguzi inachafuliwa na mizengwe, upendeleo au mifumo isiyo na usawa.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa ujumla, jitihada za Waziri Makonda zinapaswa kuangaliwa kwa jicho chanya. Lengo lake linaonekana kuwa ni kuondoa mfumo wa \u201cbora liende\u201d ambao kwa miaka mingi umeikwamisha michezo ya Tanzania, kuua vipaji na kuifanya sekta yenye nafasi kubwa ibaki kuwa ya migogoro badala ya maendeleo.<\/p>\n\n\n\n<p>Na kama kweli atasimamia alichokisema kwa vitendo, basi si ajabu kusema: huenda Waziri Makonda ameivaa \u201ckofia ya unabii\u201d katika sekta ya michezo\u2014kofia ya mtu aliyeingia kusafisha, kusahihisha na kuanzisha enzi mpya ya uwajibikaji na uwazi.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>WAUMINI wa dini mbili kubwa nchini, Uislam na Ukristo, wanaweza kukubaliana kwa urahisi kwamba manabii (mitume) walitumwa katika jamii zilizokuwa zimezama kwenye maovu na kupoteza mwelekeo wa maisha. Kusudio lao halikuwa tu kuhimiza ibada sahihi, bali kurekebisha mwenendo wa jamii kwa ujumla, kuijenga kimaadili, kiuchumi na kijamii. Katika simulizi za Qur\u2019an na Biblia, tunakumbushwa mfano [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9696,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[80],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9695","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-makala"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/maxresdefault.jpg?fit=1280%2C720&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9695","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9695"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9695\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9697,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9695\/revisions\/9697"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9696"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9695"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9695"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9695"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9695"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}