{"id":9612,"date":"2026-04-15T13:40:03","date_gmt":"2026-04-15T13:40:03","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9612"},"modified":"2026-04-15T13:40:07","modified_gmt":"2026-04-15T13:40:07","slug":"usiyoyajua-kuhusu-kocha-aliyeandika-historia-bundesliga","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9612","title":{"rendered":"USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA"},"content":{"rendered":"\n<p><strong><em>MUNICH, Ujerumani<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa kocha wa klabu ya Ligi Kuu (Bundesliga).<\/p>\n\n\n\n<p>Eta mwenye umri wa miaka 34, aliajiriwa na Union Berlin kuchukua nafasi ya Steffen Baumgart aliyefungashiwa virago. Ataiongoza timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.<\/p>\n\n\n\n<p>Eta mwenye umri wa miaka 34, si tu ameweka rekodi Bundesliga, bali pia ndiye mwanamke pekee kuwahi kuinoa timu ya wanawaume katika Ligi Kuu zote tano za Ulaya.<\/p>\n\n\n\n<p>SAFARI YAKE<\/p>\n\n\n\n<p>Kabla ya kupewa kibarua hicho, Eta alikuwa kocha wa timu ya vijana wa kiume wenye umri chini ya miaka 19 ya klabu hiyo. Pia, hii si mara ya kwanza kufanya kazi na timu ya wakubwa ya wanaume.<\/p>\n\n\n\n<p>Kuanzia mwaka 2023-2024, bibiye huyo alikuwa msaidizi wa Marco Grote baada ya Union Berlin kumfuta kazi Urs Fischer. Kocha mpya alipokuja, Nenad Bjelica, Eta aliendelea kuwa msaidizi wake.<\/p>\n\n\n\n<p>MAJERAHA YALIMKIMBIZA UWANJANI<\/p>\n\n\n\n<p>Aliwahi kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake ya Ujerumani na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010 akiwa na Turbine Potsdam.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia, Eta alikuwa sehemu ya kikosi cha U-15, U-17, U-20 na U-23 za Ujerumani, akitwaa mataji ya Euro (2008) na Kombe la Dunia (2010).<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, licha ya kiwango bora na mafanikio makubwa, alilazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 26 tu kutokana na mfululizo wa majeraha.<\/p>\n\n\n\n<p>Alimaliza masomo ya leseni ya ukocha ya UEFA Pro mwaka 2023, hivyo kuwa na sifa ya kuongoza benchi la ufundi katika klabu yoyote ya Ligi Kuu kwa upande wa wanaume.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa kocha wa klabu ya Ligi Kuu (Bundesliga). Eta mwenye umri wa miaka 34, aliajiriwa na Union Berlin kuchukua nafasi ya Steffen Baumgart aliyefungashiwa virago. Ataiongoza timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26. Eta mwenye [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":9613,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[215],"tags":[],"coauthors":[201],"class_list":{"0":"post-9612","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/WhatsApp-Image-2026-04-15-at-8.36.15-AM.jpeg?fit=399%2C221&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9612","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9612"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9612\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9614,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9612\/revisions\/9614"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9613"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9612"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9612"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9612"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9612"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}