{"id":9603,"date":"2026-04-15T13:30:30","date_gmt":"2026-04-15T13:30:30","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9603"},"modified":"2026-04-15T13:30:33","modified_gmt":"2026-04-15T13:30:33","slug":"simu-yako-chanzo-cha-ugonjwa-wa-moyo-saratani","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9603","title":{"rendered":"SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?"},"content":{"rendered":"\n<p>UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na &#8216;laini&#8217; (sim cards) zaidi ya milioni 75, kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, bado tafiti mbalimbali zinakumbusha kuwa matumizi ya simu yaliyopitiliza yanaweza kusababisha athari za kiafya, yakiwamo magonjwa ya saratani na moyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Mathalan, utafiti wa mwaka 2024 uliochapishwa katika Jarida la Cardiology nchini Canada ulibaini kuwa matumizi ya simu yaliyopitiliza yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani, Robert F. Kennedy, amekuwa mkosoaji mkubwa wa matumizi ya simu kwa kile alichodai kuwa mionzi iliyopo kwenye chombo hicho cha mawasiliano ni hatari kwa afya za watumiaji.<\/p>\n\n\n\n<p>Kupitia Kampeni yake ya &#8216;Make America Healthy Again&#8217;, Kennedy amesema baadhi ya shule nchini Marekani zimedhibiti matumizi ya simu kwa wanafunzi ili kulinda afya za watoto.<\/p>\n\n\n\n<p>Kennedy Jr. anasema mionzi ya simu, sambamba na ile ya minara ya 5G, ina athari kubwa, ikiwamo kusababisha saratani. Katika mahojiano yake na Jarida la USA Today, alisema kuna tafiti zaidi ya 10,000 zilizothibitisha hilo.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Dkt. Herbert Newton, ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Saratani cha Chuo Kikuu cha Hospitals cha Ohio, anasema:<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Simu zina kiwango kidogo sana cha mionzi, hivyo hakuna ushahidi wa moja moja kuthibitisha matumizi ya kifaa hicho yanaweza kusababisha saratani.&#8221;<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, akisisitiza uwepo wa mionzi, japo kwa kiwango kidogo, Dkt. Newton anashauri ni bora kwa mtumiaji wa simu kupendelea zaidi &#8216;kuchati&#8217; au kutumia spika ya nje (loud speaker) kuliko kuweka simu sikioni.<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati huo huo, Dkt. Newton anahimiza kufanyika kwa tafiti za kutosha kujua uhusiano uliopo kati ya matumizi ya simu na athari za kiafya.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Taasisi ya Saratani ya Marekani (NIC) inasema kama simu zinatiliwa shaka, basi hata kompyuta, runinga n &#8216;ruta&#8217; za Wifi nazo hazifai kwa kuwa nazo zina mionzi.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, utafiti wa mwaka 2024 uliofanywa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) uliohusisha watu zaidi ya 5,000, ulibaini kuwa hakuna uhusiano kati ya utumizi wa simu na saratani ya ubongo.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata waliohojiwa na kukiri kutumia simu kwa kipindi kirefu cha miaka 10, nao hawakuonekana kuwa na tatizo hilo la kiafya.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na &#8216;laini&#8217; (sim cards) zaidi ya milioni 75, kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA). Hata hivyo, bado tafiti mbalimbali zinakumbusha kuwa matumizi ya simu yaliyopitiliza yanaweza kusababisha athari za kiafya, yakiwamo magonjwa ya saratani na moyo. [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":9604,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[256,80],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-9603","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-afya","8":"category-makala"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/1b5b02f2-263e-466b-938c-4d952e0eadbb.jpeg?fit=588%2C309&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9603","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9603"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9603\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9605,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9603\/revisions\/9605"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9604"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9603"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9603"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9603"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9603"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}