{"id":9579,"date":"2026-04-15T13:08:54","date_gmt":"2026-04-15T13:08:54","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9579"},"modified":"2026-04-15T13:08:57","modified_gmt":"2026-04-15T13:08:57","slug":"watumishi-wapya-wa-ofisi-ya-taifa-ya-mashtaka-watakiwa-kuzingatia-maadili-ya-utumishi-wa-umma","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9579","title":{"rendered":"WATUMISHI WAPYA WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA"},"content":{"rendered":"\n<p>Watumishi wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwananchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainabu Athman Katambi (Mb), wakati akifungua mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya 162 wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Lush Garden, mkoani Arusha.<\/p>\n\n\n\n<p>Mhe. Katambi amesema watumishi hao wanapaswa kutumia taaluma zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cTunatarajia kuona watumishi waadilifu, wenye kufanya kazi kwa weledi na umahiri, wakizingatia misingi ya uadilifu na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa haki kwa maslahi mapana ya Taifa,\u201d amesema.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, amesisitiza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni mhimili muhimu katika kusimamia utekelezaji wa haki nchini, hivyo kuna umuhimu wa kuimarisha taasisi hiyo ili iendelee kusimamia haki jinai kwa ufanisi zaidi.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Sylvester Mwakitalu, amesema waajiriwa hao wapya wanatarajiwa kufanya kazi katika ofisi za wilaya mbalimbali nchini, ambapo hadi sasa kuna ofisi 118 zilizoanzishwa kufuatia juhudi za Serikali za kuimarisha huduma za mashtaka.<\/p>\n\n\n\n<p>Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya maadili ya utumishi wa umma na kuwapa uelewa wa kina kuhusu majukumu yao ya kila siku ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa haki.<\/p>\n\n\n\n<p>Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha sekta ya sheria kwa kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na weledi, ufanisi na wanazingatia misingi ya haki katika kuwahudumia wananchi.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Watumishi wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwananchi. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainabu Athman Katambi (Mb), wakati akifungua mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya 162 [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":12,"featured_media":9580,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[255],"class_list":{"0":"post-9579","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9579","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/12"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9579"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9579\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9581,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9579\/revisions\/9581"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9580"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9579"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9579"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9579"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9579"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}