{"id":955,"date":"2021-01-14T14:20:00","date_gmt":"2021-01-14T14:20:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/01\/14\/tanzania-inunue-petroli-iweke-akiba\/"},"modified":"2021-01-14T14:20:00","modified_gmt":"2021-01-14T14:20:00","slug":"tanzania-inunue-petroli-iweke-akiba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=955","title":{"rendered":"TANZANIA INUNUE PETROLI IWEKE AKIBA"},"content":{"rendered":"<p>\u00a0<\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/535e8-kumi2b3.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"224\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/535e8-kumi2b3.jpg?resize=400%2C224&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/div>\n<p><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">NA GEORGINA ROESER<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">BEI ya Petroli iimeshuka. Iko chini sana karibu duniani kote. Hii ilitokana na uzalishwaji mkubwa wa mafuta huko Urusi na Saudi Arabia.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Mataifa haya mawili yana msuguano wa kibiashara unaohusu bei ya mafuta. Kwa sababu ya msuguano huo, mataifa haya kila moja liliamua kuzalisha mafuta zaidi ya maradufu ya uzalishaji wake wa kawaida. Hapa ndipo neema ya kushuka kwa bei ya mafuta kwa mataifa yasiyozalisha nishati hiyo ilipoanzia. Vita vya panzi, kuku wanapeta. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump hakuupenda msuguano huo kwa sababu taifa lake kwa sasa ni miongoni mwa mataifa yenye mafuta mengi duniani.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Historia inaonyesha kuwa Marekani imekuwa ikipigana vita katika mataifa mbalimbali ya Ghuba kwa miaka nenda rudi na kupora mafuta yake.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Uporaji huo wa Marekani ndiyo ulioiwezesha kuwa na hazina kubwa ya mafuta. Hivi sasa Marekani ina jeuri ya kukaa meza moja na wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani kama Urusi na Saudi Arabia baada ya kujilimbikizia bidhaa hiyo kwa njia ya uporaji.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Tukiachana na hilo. Ukweli mwingine ni kwamba Wamarekani wengi waliwekeza katika biashara ya mafuta baada ya biashara zao za vita kuanguka hivyo wana hazina kubwa sana ya Nishati hiyo waliyopora Mashariki ya Kati.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Tangu Urusi na Saudi Arabia wamwage mafuta kedekede duniani, Marekani ilianza kupoteza mapato kutokana na bei ya mafuta kuwa chini sana miezi ya hivi karibuni. Wafanyabiashara wengi wa mafuta Marekani walikuwa wakilalamikia sana hali hiyo mwishoni mwa mwaka jana na mapema Mwaka huu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kabla ya kivumbi cha Corona, Rais Trump alitangaza kuwa ataomba &#8216;poo&#8217; kwa Urusi na Saudi Arabia waache kufanya uzalishaji mkubwa wa mafuta ili bei ipande Wamarekani waweze kuuza mafuta yao kwa bei ya juu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Urusi na Saudi Arabia walikubali kujadili kilio hicho cha Rais Trump lakini kabla ya kutekeleza hilo Corona ikabisha hodi. Sijui mazungumzo yalipoishia lakini bei ya mafuta sasa IPO chini<span>\u00a0 <\/span>kila kona ulimwenguni. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kufupisha mjadala huu ni kwamba Corona ikishaondoka vichwani vya watu, kuna uwezekano Urusi na Saudi Arabia wakafanya uzalishaji mkubwa ili kujipatia kipato cha kupambana na madhara ya Corona kiuchumi. Hili likifanyika litakuwa neema kubwa duniani kote. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa upande mwingine kuna uwezekano pia Rais Trump akawalipa fedha nzuri sana tu Urusi na Saudi Arabia wasizalishe<span>\u00a0 <\/span>kwa<span>\u00a0 <\/span>wingi mafuta yao ili bei ipande, Marekani iuze kwa bei kubwa mafuta yake.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Marekani iko tayari kutoa kiasi kikubwa kwa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani kwa sababu haiwezi kuuza mafuta yake kwa bei ya chini kama Urusi na Saudi Arabia kwa sababu mafuta yake iliyapata kwa gharama kubwa sana wakati mataifa yanayozalisha yenyewe yanachimba tu. Hii ndiyo sababu Marekani inataka bei ipande wakati wote.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Upo uwezekano Urusi na Saudi Arabia zitampuuza Rais Trump lakini hilo hatupaswi kulizingatia sana kwa sababu lolote lile linawezekana kutokea.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Sasa nini dunia inayoendelea ikiwemo Tanzania, inapaswa kufanya wakati kama huu?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kati ya mambo ambayo Afrika inapaswa kuiga kutoka Marekani; cha kwanza ni choo na mfumo wa maji taka.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Nikiri kuwa nikiwa mkazi wa hapa, vyoo vyao ni vizuri sana. Tunapaswa<span>\u00a0 <\/span>kuanza kuiga hilo siyo ule upuuzi<span>\u00a0 <\/span>wao wa uhuru wa vyombo vya habari, haki za binadamu na Demokrasia.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Hapa kwenye mafuta tunapaswa kuiga pia. Tunapaswa kufanya vile vile kama walivyofanya Marekani. Lakini sisi tusiende kupora bali tukanunue na tuweke hazina kubwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u00a0<\/span>Huu ni wakati muafaka kwa nchi yetu kununua mafuta na kuyahifadhi kama ambavyo Marekani ilifanya miaka ya nyuma. Tukanunue kwa bei poa ya sasa na tuyahifadhi kama Marekani walivyofanya. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Hatujui tunakoelekea bei itakuwaje. Kuwa na akiba ya kutosha ya mafuta ni jambo la kuzingatiwa. Nchi kama yetu ikibidi hata tutakope Urusi au Saudi Arabia mafuta mengi hivi sasa bei ikiwa chini ili baadaye tusije kupoteza fedha nyingi bei itakapopanda.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kama tuna fedha taslimu ni vema tulipie mzigo wrote tutakaonunua lakini hata kama tumepungukiwa tukakope tu hayo mafuta. Urusi kwa mfano ni marafiki zetu sana, hawatatunyima. Saudi Arabia pia hawatatunyima. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kuna uwezekano mkubwa bei ya mafuta itapanda siku chache zijazo kwa sababu nilizozieleza hapo juu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Marekani ina ushawishi mkubwa duniani kibiashara. Urusi na Saudi Arabia watahitaji fedha baada ya Corona. Marekani kwa ninavyowafahamu watawalipa Urusi na Saudia mabilioni wapunguze uzaliahaji.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Wakati ni huu. Binafsi naiona hii ni fursa kubwa sana inayoweza kupaisha uchumi wetu tukichanga karata zetu vema.<\/span><span style=\"font-size:36pt;\"><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span><span>\u00a0<\/span>.<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>\u00a0 NA GEORGINA ROESER BEI ya Petroli iimeshuka. Iko chini sana karibu duniani kote. Hii ilitokana na uzalishwaji mkubwa wa mafuta huko Urusi na Saudi Arabia. Mataifa haya mawili yana msuguano wa kibiashara unaohusu bei ya mafuta. Kwa sababu ya msuguano huo, mataifa haya kila moja liliamua kuzalisha mafuta zaidi ya maradufu ya uzalishaji wake [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[36],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-955","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-mahojiano"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/955","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=955"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/955\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=955"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=955"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=955"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=955"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}