{"id":9546,"date":"2026-04-14T12:25:39","date_gmt":"2026-04-14T12:25:39","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9546"},"modified":"2026-04-14T12:25:41","modified_gmt":"2026-04-14T12:25:41","slug":"miradi-600-yasajiliwa-ndani-ya-miaka-mitano-zanzibar","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9546","title":{"rendered":"MIRADI 600 YASAJILIWA NDANI YA MIAKA MITANO -ZANZIBAR"},"content":{"rendered":"\n<p>Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imepokea ujumbe wa maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ukiongozwa na Balozi Mkazi, Shigeki Komatsubara, katika kikao kilichofanyika Ofisi za ZIPA, Maruhubi, Mjini Magharibi Unguja.<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Saleh Saad Mohamed, alisema mamlaka hiyo imepata mafanikio makubwa katika kuvutia uwekezaji ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita, ambapo zaidi ya miradi 600 imesajiliwa yenye thamani ya takribani dola za Kimarekani bilioni 6.9.<\/p>\n\n\n\n<p>Alieleza kuwa Zanzibar imeendelea kuwa kivutio muhimu cha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hususan kutoka mataifa ya Asia ikiwemo Japan, kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yanayoendelea kuboreshwa.<br>Aidha, alibainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZIPA inaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, wakiwemo UNDP, kwa lengo la kuongeza uwekezaji katika sekta za viwanda, uchumi wa buluu pamoja na maendeleo ya rasilimali watu.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Balozi Mkazi wa UNDP, Shigeki Komatsubara, aliipongeza ZIPA kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kuvutia uwekezaji na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza uchumi jumuishi na endelevu.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilijadili fursa mbalimbali za uwekezaji, ikiwemo maendeleo ya eneo la viwanda la Mangapwani, ambalo linatarajiwa kuwa kitovu kikubwa cha ukuaji wa uchumi kupitia uwekezaji wa kimkakati.<br>Vilevile, walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika tafiti, mafunzo na ubunifu ili kuongeza thamani ya rasilimali zilizopo Zanzibar na kukuza ushindani katika soko la kimataifa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imepokea ujumbe wa maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ukiongozwa na Balozi Mkazi, Shigeki Komatsubara, katika kikao kilichofanyika Ofisi za ZIPA, Maruhubi, Mjini Magharibi Unguja. Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Saleh Saad Mohamed, alisema mamlaka hiyo imepata mafanikio makubwa katika kuvutia uwekezaji [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":12,"featured_media":9547,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[255],"class_list":{"0":"post-9546","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9546","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/12"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9546"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9546\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9548,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9546\/revisions\/9548"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9547"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9546"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9546"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9546"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9546"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}