{"id":9511,"date":"2026-04-13T15:42:23","date_gmt":"2026-04-13T15:42:23","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9511"},"modified":"2026-04-13T15:45:34","modified_gmt":"2026-04-13T15:45:34","slug":"nidhamu-kwa-wanafunzi-kumuenzi-sokoine-dc-monduli","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9511","title":{"rendered":"WANAFUNZI MONDULI WAHIMIZWA NIDHAMU KUMUENZI SOKOINE"},"content":{"rendered":"\n<p>Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Gloriana Kimath amemtaja Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha Hayati Edward Moringe Sokoine kama Kiongozi muadilifu, mzalendo, asiyekuwa mbinafsi na mwenye kushughulika na masuala ya watu, akihimiza nidhamu kwa wanafunzi ili kuweza kufikia malengo na ndoto walizonazo.<\/p>\n\n\n\n<p>Gloriana ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha Bonanza la Michezo lililokutanisha Shule Tano za Sekondari zinazotoka kwenye Kata za Monduli Mjini na Engutoto zilizoshiriki michezo ya mpira wa kikapu, mpira wa miguu, mikono na mpira wa pete, bonanza lililoandaliwa na Taasisi ya Sokoine Foundation kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 42 ya kifo cha Waziri Mkuu huyo wa zamani.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cLeo hii tunaadhimisha miaka 42 tangu kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine. Hayati Sokoine alikuwa Kiongozi anayeshughulika na mambo ya wananchi kwa lugha rahisi hakukuwa mbinafsi, hakukuwa Kiongozi wa kujinufaisha mwenyewe, alisimamia maslahi ya wananchi anaowaongoza.<br>Niwaombe tuzingatie nidhamu katika kufikia malengo, nidhamu inaanzia shuleni na huwezi kuwa Kiongozi muadilifu ikiwa hukua na tabia nzuri shuleni.\u201d Amesema Gloriana.<\/p>\n\n\n\n<p>Gloriana ametumia hotuba yake pia kuwasihi wanafunzi hao kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao kama ilivyokuwa kwa hayati Sokoine pamoja na kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao kikamilifu.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika Bonanza hilo lililofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Moringe na kuhusisha shule za Sekondari Moringe Sokoine, Engutoto, Irkisongo na Shule ya Sekondari Alfa Omega, Gloriana Kimath alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Fedha Taslimu, Medali na Makombe.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Gloriana Kimath amemtaja Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha Hayati Edward Moringe Sokoine kama Kiongozi muadilifu, mzalendo, asiyekuwa mbinafsi na mwenye kushughulika na masuala ya watu, akihimiza nidhamu kwa wanafunzi ili kuweza kufikia malengo na ndoto walizonazo. Gloriana ametoa kauli hiyo wakati [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":12,"featured_media":9512,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[255],"class_list":{"0":"post-9511","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9511","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/12"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9511"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9511\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9515,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9511\/revisions\/9515"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9512"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9511"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9511"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9511"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9511"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}