{"id":9484,"date":"2026-04-13T15:17:48","date_gmt":"2026-04-13T15:17:48","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9484"},"modified":"2026-04-13T15:17:50","modified_gmt":"2026-04-13T15:17:50","slug":"dc-mkude-asisitiza-umuhimu-wa-usafirishaji-katika-utoaji-huduma-za-umeme","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9484","title":{"rendered":"DC MKUDE ASISITIZA UMUHIMU WA USAFIRISHAJI KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA UMEME"},"content":{"rendered":"\n<p>Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Modest Mkude, amesema kuwa sekta ya usafirishaji na lojistiki ni nguzo muhimu katika kuhakikisha upatikanaji na utoaji bora wa huduma za umeme kwa wananchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Amesema bila kuwepo kwa mifumo imara ya usafirishaji, inakuwa vigumu kufikisha huduma kwa wakati, hususan katika maeneo ya vijijini na yale yenye changamoto za miundombinu.<\/p>\n\n\n\n<p>Mhe. Mkude aliyasema hayo leo Jumapili, Aprili 13, 2026 jijini Arusha, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Maafisa Usafirishaji na Lojistiki wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aliwahimiza washiriki kutumia vyema mafunzo wanayopata ili kuboresha usimamizi wa rasilimali wanazotumia katika utekelezaji wa majukumu yao.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, amesisitiza umuhimu wa majadiliano yenye tija, akieleza kuwa ana imani mkutano huo utachochea ari mpya ya utendaji kazi kwa weledi zaidi kwa manufaa ya taifa.<\/p>\n\n\n\n<p>Amesema mkutano huo ni fursa muhimu ya kujenga uelewa wa pamoja, kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha sekta ya usafirishaji ndani ya TANESCO.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika hatua nyingine, Mhe. Mkude amesema serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza katika ununuzi wa vitendea kazi vya sekta hiyo. Amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2025\/2026, jumla ya Shilingi bilioni 180 zilitumika kununua vyombo vya usafiri 802. Vilevile, Shilingi bilioni 200 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2026\/2027 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vingine vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa magari na vifaa vya usafiri vinavyonunuliwa na serikali, akibainisha kuwa vinagharimu fedha nyingi hivyo ni lazima vitunzwe na kutumika kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Modest Mkude, amesema kuwa sekta ya usafirishaji na lojistiki ni nguzo muhimu katika kuhakikisha upatikanaji na utoaji bora wa huduma za umeme kwa wananchi. Amesema bila kuwepo kwa mifumo imara ya usafirishaji, inakuwa vigumu kufikisha huduma kwa wakati, hususan katika maeneo ya vijijini na yale yenye changamoto za [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":12,"featured_media":9485,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[255],"class_list":{"0":"post-9484","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9484","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/12"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9484"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9484\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9486,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9484\/revisions\/9486"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9485"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9484"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9484"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9484"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9484"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}