{"id":9464,"date":"2026-04-13T13:10:06","date_gmt":"2026-04-13T13:10:06","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9464"},"modified":"2026-04-13T13:10:08","modified_gmt":"2026-04-13T13:10:08","slug":"tff-na-bmt-kuimarisha-vyama-vya-mpira-wa-miguu-tanzania","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9464","title":{"rendered":"TFF NA BMT KUIMARISHA VYAMA VYA MPIRA WA MIGUU TANZANIA"},"content":{"rendered":"\n<p>fisa Masoko wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Hannah Kassimoto, mwishoni mwa wiki iliyopita alikutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Mohamed Mkangara, kwa lengo la kujadili namna ya kuimarisha utendaji na uhai wa vyama vya mpira wa miguu katika ngazi ya mkoa na wilaya.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zilijadili mikakati ya ushirikiano itakayosaidia kuviwezesha vyama vilivyo chini ya shirikisho hilo kushirikiana na vyama vya mikoa na wilaya, kwa lengo la kuboresha uwezo wa kiutawala, kiutendaji na kifedha.<\/p>\n\n\n\n<p>Moja ya ajenda kuu iliyojadiliwa ni umuhimu wa viongozi wa vyama hivyo kulipa ada za mwaka zinazotozwa na BMT. Ilielezwa kuwa ulipaji wa ada hizo ni sehemu ya matakwa ya kisheria na msingi muhimu katika kuimarisha uendeshaji wa michezo nchini. Aidha, ada hizo huchangia katika udhibiti, usimamizi na maendeleo ya sekta ya michezo katika ngazi mbalimbali.<\/p>\n\n\n\n<p>Bi. Kassimoto alisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za usajili na ulipaji wa ada ili kuhakikisha vyama vinatambuliwa rasmi na kupata uhalali wa kuendesha shughuli za mpira wa miguu katika maeneo yao.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Bw. Mkangara alieleza kuwa TFF itaendelea kushirikiana kwa karibu na BMT ili kuhakikisha vyama vya mikoa na wilaya vinafuata matakwa yote ya kisheria. Pia aliahidi kuwa shirikisho hilo litaongeza juhudi katika kutoa elimu kwa wanachama wake ili kuboresha uendeshaji wa vyama hivyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya michezo nchini kupitia usimamizi bora na ushirikiano wa taasisi husika.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>fisa Masoko wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Hannah Kassimoto, mwishoni mwa wiki iliyopita alikutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Mohamed Mkangara, kwa lengo la kujadili namna ya kuimarisha utendaji na uhai wa vyama vya mpira wa miguu katika ngazi ya mkoa na wilaya. Katika mazungumzo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":12,"featured_media":9465,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[216],"tags":[],"coauthors":[255],"class_list":{"0":"post-9464","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo-kitaifa"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9464","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/12"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9464"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9464\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9466,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9464\/revisions\/9466"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9465"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9464"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9464"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9464"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9464"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}