{"id":9401,"date":"2026-04-11T14:03:54","date_gmt":"2026-04-11T14:03:54","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9401"},"modified":"2026-04-11T14:03:58","modified_gmt":"2026-04-11T14:03:58","slug":"kinachoendelea-mkutano-wa-amani-kati-ya-marekani-iran","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=9401","title":{"rendered":"KINACHOENDELEA MKUTANO WA AMANI KATI YA MAREKANI, IRAN"},"content":{"rendered":"\n<p>ISLAMABAD, Pakistan<\/p>\n\n\n\n<p>PAKISTAN ndiyo mwenyeji wa mazungumzo ya kutafuta suluhu katika mgogoro unaoendelea kati ya Iran na Marekani inayoshirikiana na Israel.<\/p>\n\n\n\n<p>Mazungumzo hayo yaliyotanguliwa na makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki mbili, yanakuja zikiwa ni wiki sita tangu Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran.<\/p>\n\n\n\n<p>Mashambulizi yaliyosababisha aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo la Kiarabu, Ayatollah Ali Khamenei.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande mwingine, vita hivyo vimesababisha athari kubwa kiuchumi, ikiwamo kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta duniani kote.<\/p>\n\n\n\n<p>Kupanda kwa bei kulitokana na hatua ya Iran kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao asilimia 20 ya mafuta na gesi duniani hupita hapo.<\/p>\n\n\n\n<p>Sasa, mazungumzo yaliyotatajiwa kuanza leo Aprili 10, 2026 yanafanyika mjini Islamabad, kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif.<\/p>\n\n\n\n<p>HOTELI YA MAZUNGUMZO, WAANDISHI WA HABARI 20 TU<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mujibu wa taarifa, mazungumzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Serena mjini Islamabad, jirani na ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, na yanaweza kuchukua hadi siku 15.<\/p>\n\n\n\n<p>Kutokana na uzito wa mazungumzo hayo, mamlaka za Pakistan zimetangaza siku mbili za mapumziko ya kitaifa, isipokuwa kwa vyombo vya dola na madaktari.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wa Marekani, uwakilishi wao utaongozwa na Rais Donald Trump, na Makamu wa Rais, JD Vance.<\/p>\n\n\n\n<p>Ujumbe wa Iran utaongozwa na Spika wa Bunge, Mohammad Bagher Ghalibaf, na Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araghchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Waziri Mkuu wa Pakistan, Sharif, ndiye anayeongoza mazungumzo, ikiwamo kukutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa pande zote mbili.<\/p>\n\n\n\n<p>Awali, taarifa zilieleza kuwa wawakilishi wa Iran na Marekani wasingekaa chumba kimoja, na badala yake wangewasiliana kupitia maofisa wa Pakistan.<\/p>\n\n\n\n<p>Ikaelezwa pia, vyombo vya habari vya kimataifa zaidi ya 30 vilifanya maombi ya kuhudhuria Mkutano huo lakini ni waandishi 20 pekee waliokubaliwa.<\/p>\n\n\n\n<p>KWANINI PAKISTAN KATIKATI YA MGOGORO?<\/p>\n\n\n\n<p>Pakistan ni majirani wa Iran. Ni umbali wa kilometa 900 pekee unaotenganisha mataifa hayo ya Mashariki ya Kati.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia, tofauti na mataifa mengi ya Mashariki ya Kati, Pakistan haina kambi za kijeshi za Marekani, na hiyo inaipa sifa ya upekee mbele ya macho ya Iran.<\/p>\n\n\n\n<p>Vilevile, baada ya Iran, Pakistan ndiyo nchi ya Kiarabu yenye idadi kubwa zaidi ya Waislam wa dhehebu la Shia.<\/p>\n\n\n\n<p>Kama hiyo haitoshi, kwa sasa Marekani haina balozi ndani ya ardhi ya Pakistan tangu mwaka 2025.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, hakuna Rais wa Marekani aliyeitembelea Pakistan tangu George W. Bush alipofanya hivyo mwaka 2006.<\/p>\n\n\n\n<p>Sababu hizo, pamoja na zingine zinazoweza kuwapo, zinaifanya Iran isiwe na wasiwasi na Pakistan.<\/p>\n\n\n\n<p>MAZUNGUMZO YATAMALIZA VITA MASHARIKI YA KATI?<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa wachambuzi wa siasa za ulimwengu, bado ni ngumu kutarajia mazungumzo hayo kumaliza vita moja kwa moja.<\/p>\n\n\n\n<p>Mjumbe wa Iran mjini Islamabad, Amiri Moghadam, amesema kitendo cha Israel kuendelea kuishambulia Lebanon kinafifisha matumaini ya kupatika kwa suluhu ya kudumu.<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati huu Marekani na Iran zikiwa mezani, vikosi vya Israel vinashambuliana na wapiganaji wa Hezbollah huko Lebanon.<\/p>\n\n\n\n<p>Ifahamike kuwa Hezbollah wako upande wa Iran na waliingia vitani baada ya kuona &#8216;marafiki&#8217; zao hao wanashambuliwa na Marekani na Israel.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa wachambuzi, kitendo cha Rais Trump kusema Lebanon kushambuliwa haihusiani na mazungumzo ya amani kimebariki Israel iendeleze uharibifu, jambo ambalo Iran haiwezi kulikubali.<\/p>\n\n\n\n<p>Hivyo, wachambuzi wanaamini Lebanon na Israel, kwa namna moja au nyingine, zilipaswa kuwa sehemu ya mazungumzo ya amani ili kupata suluhu ya kudumu katika mgogoro wa Mashariki ya Kati.<\/p>\n\n\n\n<p><strong><em>Imeandaliwa na Hassan Mwasha, kwa msaada wa Mashirika mbalimbali ya Habari<\/em><\/strong><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>ISLAMABAD, Pakistan PAKISTAN ndiyo mwenyeji wa mazungumzo ya kutafuta suluhu katika mgogoro unaoendelea kati ya Iran na Marekani inayoshirikiana na Israel. Mazungumzo hayo yaliyotanguliwa na makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki mbili, yanakuja zikiwa ni wiki sita tangu Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran. Mashambulizi yaliyosababisha aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo la [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":9402,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[74,81],"tags":[],"coauthors":[201],"class_list":{"0":"post-9401","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kimataifa","8":"category-makala-kimataifa"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9401","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=9401"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9401\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9403,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/9401\/revisions\/9403"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/9402"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=9401"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=9401"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=9401"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=9401"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}