{"id":911,"date":"2021-01-23T08:47:00","date_gmt":"2021-01-23T08:47:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/01\/23\/kesi-ya-heroin-ya-muna-hariri-nani-wa-kumfunga-paka-kengele\/"},"modified":"2022-11-09T11:39:06","modified_gmt":"2022-11-09T11:39:06","slug":"kesi-ya-heroin-ya-muna-hariri-nani-wa-kumfunga-paka-kengele","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=911","title":{"rendered":"KESI YA HEROIN YA MUNA, HARIRI NANI WA KUMFUNGA PAKA KENGELE?"},"content":{"rendered":"<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/00ac4-2.png\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"390\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/00ac4-2.png?w=300\" width=\"400\"><\/a><\/div>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">NA CHARLES MULLINDA<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">BADO sijamuona mtu wa kumfunga paka kengele ili kutanzua mtanziko uliopo sasa katika mjadala mkali unaohusu kushindwa kwa serikali katika kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa ikiwakabili wapenzi wawili, Mohamed Hariri na Muna Said.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Ninachokiona ni hofu, wasiwasi, woga, vitisho na upigaji ramli. Niliowaalika kujibu maswali mepesi yanayoulizwa sasa na wachokonozi huku uswahilini hawajajitokeza hata mmoja. Wote wamenyaza.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Walisoma maandishi ya mchokonozi na kuyaelewa vema maswali mepesi aliyowauliza makachero wa kesi ya unga ya Muna na Hariri kisha wakanyamaza. Wakanyamaza kimya kabisa. Kimya cha msibani.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Waliojitokeza ni wapiga porojo. Baadhi wameeleza mshangao wao kwa kusoma maandishi ya kichokonozi yakiwa na maswali mepesi ambayo eti! Hayajibiki!<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Eti, kwao wao maandishi hayo ya kichokonozi hayakupaswa kuandikwa katika jukwaa hili na kusomwa na maelfu ya watu kwa sababu kufanya hivyo ni kuwaanika wahusika.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Wengine wamejitokeza wakichekea kwapani huku wakigongeana viganja vya mikono yao kwa furaha ya kusoma andiko linalofikirisha. Eti! wanaulizana mchokonozi ni nan!? Watu wa ajabu sana.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Wapo walioogopa na kunivaa wazima wazima kwa sauti zilizojaa hofu zilizokuwa zikinong&#8217;ona kuwa ninachokoza nyuki; na wachache wamethubutu kuninyooshea kidole cha ole. Eti! Nisithubutu tena. Wanaponda kokoto kwenye chuma cha pua.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Ndiyo kwanza nimeanza kuandika, maandishi yangu ni mepesi na yanayofurahisha kuyasoma! Sina mamlaka ya kuhukumu wala sijahukumu yeyote.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Nilichofanya ni kuchangia mjadala uliohudhunisha wengi ambao msingi wake ni fedheha iliyoipata serikali kwa kushindwa mahakamani katika Kesi ya unga. Sasa weweseko ni la nini?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Muna na Hariri sasa ni raia huru baada ya kuibwaga serikali mahakamani lakini wachokonozi hawazuiliwi kusemezana kuhusu mwenendo wa kesi yao.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kesi nzito nzito na za kukata na shoka kama hii ya Muna na Hariri na kwa upande mwingine serikali, mwenendo na hukumu zake hutumiwa kufundisha vyuoni na pia hutumiwa na majaji na mahakimu kama rejea wanapohukumu watu wema na waovu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Ndivyo ilivyo hata kwa wachokonozi, Kesi hii ni darasa la kukata na shoka ambalo mwanafunzi akilielewa vizuri anaweza kujinasua katika vitanzi vigumu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Tutakuwa tunatenda dhambi ambayo haiwezi kutolewa hukumu mahakamani kama tutaanza kutapatapa kuhusu hatma ya Muna na Hariri kwa sababu tu ya mjadala unaohusu ushindi wao dhidi ya serikali.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Wanaoweweseka sasa baada ya mjadala huu kupewa hadhi ya kichokonozi ya kuwa kesi darasa wanatulazimisha wachokonozi tujiulize kuwa, kama hakukuwa na tatizo katika mwenendo mzima wa kesi hadi hukumu, kwanini wameanza kutapatapa na kujiuliza ni wapi kinakotokea kiherehere cha mchokonozi kuipa hadhi kesi hii iliyomalizika kwa kutoa ushindi kwa washitakiwa?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><\/span><\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/7baf0-unga.jpg\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"240\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/7baf0-unga.jpg?w=300\" width=\"400\"><\/a><\/div>\n<p><span style=\"font-size:large;\"><br \/>\n<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Itoshe tu kueleza msimamo wangu hapa kuwa nitaendelea kuandika kuhusu kesi hii kwa sababu sasa ninaamini zipo kesi nyingi za aina hii au zinazokuja ambazo pengine, serikali itashindwa mahakamani.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Nitaendelea kuandika ili kuitoa serikali tongotongo za macho, iweze kuona kama zipo kesi nyingine ambazo haiwezi kushinda zifutwe kuliko kuendelea nazo na mwisho kushindwa kwa&nbsp; fedheha.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa wachokonozi wenzangu, naweka agano nanyi kuwa sitakiuka makubalino yetu kwa kuendelea kuhoji maswali mepesi kabla sijapata majibu ya maswali mepesi niliyouliza siku chache zilizopita.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Sitauliza kama kile kinachozungumzwa sasa huko uswahili kuwa eti! Muna ndiye alikuwa kiungo mchezeshaji katika kesi hii na sitathubutu kuhoji popote kuwa tangu kukamatwa kwa kiungo huyo mchezeshaji, Muna, na kukaa msambweni zaidi ya mwaka mmoja alikuwa akitembelewa kila mara na kina nani?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Mchokonozi ni mtu wa agano. Nimeweka agano nanyi. Ninawaachia makachero wajiulize wenyewe na waje na majibu ni nani hasa aliyekuwa akifika gerezani mara kwa mara kumtembelea Muna? Mtu huyo alikuwa ndugu yake? rafiki yake? binamu yake wa hiari, shemeji yake au msamalia mwema?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Siyo kazi yangu kuwafundisha makachero kazi ya ukachero hivyo ninawaachia wenyewe kutafuta tarehe, mwezi na mwaka ambao Muna aliingia gerezani.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><\/span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/48e07-3.jpg\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\"><img decoding=\"async\" border=\"0\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/48e07-3.jpg?w=300\" width=\"320\"><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Mfanyabiashara Mohamedi Hariri, ambaye ameibwaga serikali mahakamani katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kukamatwa na unga pamoja na mkewe Muna Said<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-size:large;\"><br \/>\n<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Wanajua makachero na naamini watajua kama hizi tetesi za huku uswahili kwa wachokonozi kuwa kipindi chote cha Corona ambapo hakukuwa na ruhusa ya wageni kwenda magereza kusalimia, ni akina nani walikuwa wakikiuka utaratibu huo?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Haya ni maandishi ya mkono wangu mchokonozi ambayo hayataruka karatasi hii kwa sasa kwenda ya pili kuhoji ni akina nani kule gerezani waliokuwa wakitoa ruhusa kwa wageni kuingia gerezani wakati kulikuwa na zuio?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Tukutane wiki ijayo.<\/span><span style=\"font-size:24pt;\"><\/span><\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NA CHARLES MULLINDA BADO sijamuona mtu wa kumfunga paka kengele ili kutanzua mtanziko uliopo sasa katika mjadala mkali unaohusu kushindwa kwa serikali katika kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa ikiwakabili wapenzi wawili, Mohamed Hariri na Muna Said. Ninachokiona ni hofu, wasiwasi, woga, vitisho na upigaji ramli. Niliowaalika kujibu maswali mepesi yanayoulizwa sasa na wachokonozi huku [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3422,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[73],"tags":[33],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-911","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-mchokonozi","8":"tag-mchokonozi"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/911","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=911"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/911\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3424,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/911\/revisions\/3424"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3422"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=911"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=911"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=911"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=911"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}