{"id":697,"date":"2021-04-14T15:00:00","date_gmt":"2021-04-14T15:00:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/04\/14\/ripoti-ya-cag-na-haja-ya-kujitathmini\/"},"modified":"2021-04-14T15:00:00","modified_gmt":"2021-04-14T15:00:00","slug":"ripoti-ya-cag-na-haja-ya-kujitathmini-2","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=697","title":{"rendered":"RIPOTI YA CAG NA HAJA YA KUJITATHMINI"},"content":{"rendered":"<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/81483-cag.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"200\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/81483-cag.jpg?resize=400%2C200&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/p>\n<p><span style=\"background-color:white;color:#222222;font-family:Garamond, serif;font-size:x-large;\">ABBAS MWALIMU<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">0719258484<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Habari kubwa katika vyombo vya habari na mijadala inayoendelea kwenye jamii kwa sasa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere aliyoitoa kwa waandishi wa habari, Alhamisi ya Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Katika taarifa fupi ya ukaguzi aliyotoa kwa umma kupitia waandishi wa habari, CAG Kichere amebaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma na yasiyozingatia bajeti katika wizara, taasisi, wakala na idara kadhaa za serikali hali ambayo imezua mijadala na maswali mengi kutoka kwa wananchi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa mujibu wa CAG Kichere ni kwamba ofisi yake ilibaini matumizi yaliyo nje ya bajeti kwa taasisi na wakala kama vile TANROADS, TAWA, TARURA, TIA n.k, sambamba na Wizara za Maliasili na Utalii, Wizara ya Afya na Wizara ya Ujenzi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa mfano, CAG alisema\u00a0alibaini matumizi ya Shilingi milioni 172 zilizoidhinishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake kwa ajili ya kufadhili tamasha la Kigwangalla Kili Chalenji 2019 kupitia Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA) na pia kiasi cha Shilingi milioni 114 kutoka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kiasi cha Shilingi milioni 57 kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wakati shindano hilo halikuwepo kwenye bajeti za mwaka wa fedha za mamlaka hizo.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"font-size:large;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">Mbali na matumizi hayo kwa mujibu wa CAG Kichere, alibaini pia Kituo cha Utangazaji wa Clouds kililipwa Shilingi milioni 629 na <\/span><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">\u00a0<\/span><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">Shirika la Utangazaji (TBC) lilipwa Shilingi milioni 201 kwa ajili ya kuonesha matangazo ya tamasha la urithi huku Kampuni ya Wasafi ikilipwa Shilingi milioni 140 kwa ajili ya kutangaza utalii wa ndani katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Dodoma.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Ni wazi kuwa ripoti hii ya CAG imeshtua watu wengi sana na kuzua maswali kadha wa kadha ambayo nadhani yanaweza kujibiwa kwa ufasaha na wahusika.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Binafsi ripoti hii ya CAG inanifanya nidhani kuwa kuna haja kwa serikali kujenga mfumo imara wa kujitathmini kutokea ndani na kupanua uwajibikaji kwa kuongeza ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 8 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba:<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/11ddf-cag2b2.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"253\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/11ddf-cag2b2.jpg?resize=400%2C253&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akikabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-size:large;\"><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; ambapo kifungu (b) kinaeleza kuwa &#8216;lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;&#8217;<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa nini nadhani hivi?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa sababu nafikiri kuna changamoto kwenye namna ya kujifanyia tathmini kutoka kwenye mfumo uliopo sasa ambapo CAG badala ya kuwa na maamuzi yenye uwezo wa kuathiri moja kwa moja (Sanctioning\/enforcing decisions) amekuwa akishauri zaidi jambo linalotoa mwanya kwa baadhi ya Watanzania wasio waadilifu kuendelea\u00a0 kutumia ofisi za Serikali vibaya kutokana na kukosekana kwa uwazi kwenye matumizi ya fedha za umma kwa baadhi ya wizara, idara, wakala na taasisi za serikali na hivyo kurudisha nyuma dhana ya utawala bora.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Tukumbuke kuwa utawala bora ni miongoni mwa viambata vya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na katika kutekeleza hilo serikali iliunda Mpango Taifa wa Utawala Bora (NFGG) mwaka 1999 ukiwa na lengo la kuleta maisha bora kwa kuangazia maeneo saba muhimu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Licha ya mpango huo, Ofisi ya CAG ni miongoni mwa taasisi muhimu katika kuleta utawala bora na uwajibikaji nchini. Rejea Mdee na Thorley (2016), Tripp (2012) na Daima Associates (2009)\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Tukumbuke pia kuwa Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi 14 mwanachama wa Ubia wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP) tangu mwaka 2011 ilipojiunga na baadaye kujitoa mwaka 2015 ambapo Halmashauri ya Mji wa Kigoma tu ndiyo imebaki katika mpango huo wa OGP kama walivyoainisha Juma na Matuku (2019) katika andiko lao -&#8216;Towards Inclusive Open Government in Africa.\u201d<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Wakati Tanzania ilipojiunga na OGP iliweza kuja na Mpango Kazi wa Taifa (National Action Plan) au NAP wa mwaka 2012 mpaka 2016 ambapo katika mpango kazi wa awamu ya kwanza (2012-2013) Serikali ilijidhatiti kuimarisha upatikanaji wa taarifa za utendaji kazi wa Serikali katika nyanja mbalimbali.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa bahati mbaya ni malengo mawili tu kati ya malengo 25 ambayo Serikali ilijidhatiti nayo yalifikiwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"font-size:large;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">Mpango kazi wa awamu ya pili (2014-2016) ulijielekeza kwenye sheria ya kupata taarifa (information act), bajeti kuwa wazi (open budget), data kuwa wazi (open data), uwazi katika ardhi na viwanda vya uchimbaji (extractive industry). Rejea Richard\u00a0 Mabala na Kefar Mbogela katika<\/span><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">\u00a0 <\/span><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">&#8211; \u2018Evaluating and Shaping Engagement on OGP: A Case Story from Tanzania.\u2019<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Lakini kutokana na changamoto mbalimbali,\u00a0mwaka 2015 Tanzania ilijitoa katika mkataba wa OGP na kubaki kwenye Mpango wa Hiyari wa Nchi za Umoja wa Afrika Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora yaani APRM, mpango ambao kwa mujibu wa Razzano na Gruzd (2015) katika andiko lao \u2013\u2018A Next Generation Peer Review: What Does the Open Government Partnership have to offer\u2019- wanasema una michakato mingi na migumu kutelezeka.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Hivyo basi, kwa mtazamo wangu nadhani hali hii ya Ofisi ya CAG kubakia kuwa mhimili pekee madhubuti wa kujipima kutokea ndani\u00a0 imesababisha kupungua kwa wigo wa mifumo ya kujifanyia tathmini hali inayosababisha CAG kubaini changamoto nyingi katika matumizi ya fedha za walipa kodi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/7ad19-katiba.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"400\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/7ad19-katiba.jpg?resize=400%2C400&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-size:large;\"><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">NINI KIFANYIKE?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Nafikiri sasa kuna haja ya kuipandisha hadhi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwa Mamlaka kamili, yaani; Controller and Audit General Authority (CAGA).<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa nini nasema hivi? Kwa sababu kwa mtazamo wangu naamini ikiwa mamlaka kamili (Authority) itakuwa na uwezo wa kimaamuzi (ability to enforce sanctions) yatakayosababisha baadhi ya watu kuwajibishwa moja kwa moja kwa mujibu sheria itakayokuwa ikiongoza &#8216;Mamlaka&#8217; hiyo badala ya kuishia kushauri &#8216;Mamlaka&#8217; tu.\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa maoni yangu, CAG akikosa nguvu za moja kwa moja za kuathiri ama (sanctions) kisheria,\u00a0nadhani bado changamoto zitazidi kuwa kubwa na hivyo msukumo unaweza kupungua zaidi katika utawala bora na uwajibikaji wa Serikali kwa maana ya kwamba\u00a0 baadhi ya watumishi wa umma wataendelea kutokuwa waadilifu kwa nchi na wananchi na hivyo kushindwa kuwaletea ustawi wananchi huku likiwa ndiyo lengo kuu la Serikali kwa mujibu wa Katiba.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Hili liligusiwa pia na Razanno na Gruzd (2015)\u00a0 walipoeleza kwa lugha ya Kingereza kwamba, &#8220;&#8230;the lack of tough sanctions may mean that the political reputational incentive is not significant enough to warrant change&#8221;<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Tumeona mafanikio kadhaa kwa TAKUKURU tangu ilipokuwa taasisi inayojitegemea na hata Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa sana hivyo CAGA nayo itafanikiwa bila shaka.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Mbali na Ofisi ya CAG kuwa \u2018Mamlaka\u2019 kamili\u00a0 nadhani pia kuna haja ya kutazama upya mfumo wetu wa kutathmini uwazi (transparency), uwajibikaji (accountability), kupambana na rushwa (jambo ambalo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliwaagiza TAKUKURU), kuwawezesha wananchi kushiriki katika maamuzi sambamba na kuhanikiza utumiaji wa teknolojia kuimarisha utawala bora kama vile kuhakikisha miamala yote inafanyika kwa njia za kielekroniki kupitia simu ya kiganjani ili kuondoa mianya ya rushwa na ubadhilifu.?<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Katika kufikia azma hizi nadhani kuna haja ya kuwa na mfumo wa kujitathmini wa serikali ambao unaweza kuitwa \u2013\u2018Tanzania Accountability and Participation Independent Review Mechanism au TAPIRM.\u2019<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa maoni yangu nafikiri hii \u2018mechanism\u2019 ingekuwa sehemu ya CAGA katika kufanya tathmini ni kwa kiwango gani wananchi wa kawaida wanatambua wajibu wao kwa wale waliowachagua na walioteuliwa kwa lengo la kuwahudumia\u00a0 kwa sababu kwa mfano, tafiti zinaonesha kuwa baadhi ya wananchi hawana imani na Serikali za mitaa (local governments) kutokana na kuhofia kutosikilizwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Hili liliainishwa katika utafiti uliofanywa na Anna Mdee na Lisa Thorley na kuchapishwa mwezi Oktoba, 2016 uliokuwa na kichwa cha utafiti, \u2018Good governance, local government, accountability and service delivery in Tanzania: Exploring the context for creating a local governance performance index.\u2019 ambapo katika utafiti wao wamebaini kama ifuatavyo:<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">\u2018Citizens are also less likely to engage with their LGAs as there is a perception their concerns will not be heard or taken seriously.\u2019 (Mdee na Thorley, 2016:12).<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/babashadya6.files.wordpress.com\/2021\/04\/d5fed-pm.jpg\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"176\" src=\"https:\/\/babashadya6.files.wordpress.com\/2021\/04\/d5fed-pm.jpg?w=300&#038;resize=400%2C176\" width=\"400\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Waziri Mkuu, Kassin Majaliwa akiwa katika moja ya mikutano yake ya hadhara ambayo wananchi hupata nafasi ya kueleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-size:large;\"><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Huenda hii ya kukosa imani ndiyo sababu wananchi hubeba mabango pindi waonapo ama kusikia ziara ya Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika eneo lao hali iliyopelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwaonya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi ambao watabainika kuzuia haki hiyo\u00a0 ya wananchi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Hivyo basi kwa mtazamo wangu naamini ipo haja ya kuwa na \u2018mechanism\u2019 yetu wenyewe ya kutathmini uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini yaani (TAPIRM) itakayokuwa ndani ya CAGA ili wananchi washiriki katika kufanya maamuzi na kupanua wigo wa utawala bora baada ya kuwa tumejitoa OGP.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Kimsingi ninaamini kuwa kuna haja ya sisi kama Watanzania kujitathmini na kwa Serikali kuipandisha hadhi Ofisi ya CAG kuwa mamlaka inayojitegemea yaani CAGA itakayokuwa na uwezo wa kuathiri (enforcing decisions\/sanctions) kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaohusika na matumizi mabaya ya fedha za umma na ambayo itakuwa na tawi la kupima uwajibikaji (TAPIRM) kwa kuwashirikisha wananchi\u00a0 ili tufikie azma ya Dira ya Taifa 2025.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"font-size:large;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">Kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.<\/span><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\">Abbas Mwalim<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Facebook|Instagram|Twitter.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">+255 719 258 484<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"background:white;line-height:normal;margin-bottom:0.0001pt;margin-bottom:0;\"><span style=\"color:#222222;font-family:Garamond, serif;\"><span style=\"font-size:large;\">Uwanja wa Diplomasia (Facebook|WhatsApp).<\/span><span style=\"font-size:22pt;\"><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere \u00a0 ABBAS MWALIMU 0719258484 Habari kubwa katika vyombo vya habari na mijadala inayoendelea kwenye jamii kwa sasa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere aliyoitoa kwa waandishi wa habari, Alhamisi ya Aprili 8, 2021 jijini Dodoma. Katika [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[36],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-697","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-mahojiano"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/697","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=697"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/697\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=697"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=697"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=697"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=697"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}