{"id":658,"date":"2021-04-30T06:11:00","date_gmt":"2021-04-30T06:11:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/04\/30\/anayedaiwa-kujipatia-mali-za-marehemu-kwa-ulaghai-apambana\/"},"modified":"2021-04-30T06:11:00","modified_gmt":"2021-04-30T06:11:00","slug":"anayedaiwa-kujipatia-mali-za-marehemu-kwa-ulaghai-apambana","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=658","title":{"rendered":"ANAYEDAIWA KUJIPATIA MALI ZA MAREHEMU KWA ULAGHAI APAMBANA"},"content":{"rendered":"<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/452c6-urithi.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"225\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/452c6-urithi.jpg?resize=400%2C225&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/div>\n<p><\/p>\n<p><\/p>\n<p>\u00a0<span style=\"font-family:Garamond, serif;font-size:x-large;\">NA MWANDISHI WA PANORAMA<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">SAKATA la kujipatia mali kwa njia ya ulaghai linalomuandama mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Dali Yusuph Musa sasa limeanza kuibua maswali mengi yenye utata baada ya mfanyabiashara huyo kufanya mahojiano na Tanzania PANORAMA Blog na kueleza kuwa yupo tayari kwa mapambano ambayo yatamuweka huru.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Katika mahojiano hayo yaliyofanyika jana eneo la Magomeni Moroko, Dali alisema tuhuma na shutuma anazoelekezewa na baadhi ya ndugu zake kuwa amejimilikisha mali zinazohamishika na zisizohamishika za marehemu Yusuph Dali aliyefariki mwaka 2019 nchini Italia zina lengo la kumpoka haki yake ya urithi aliyopewa na marehemu baba yake kabla ya kukutwa na umauti.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Alisema amekuwa akipambana kimya kimya na wanaotaka kumpoka haki yake ya urithi katika mahakama na kwenye mabaraza ya dini ambako kote alishinda lakini anazidi kuandamwa hivyo sasa yupo tayari kusimama hadharani kupambana ili hatimaye aishi kwa amani.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Miongoni mwa mambo aliyoyatolea ufafanuzi ni tofauti ya majina yake yanayoonekana katika cheti chake za kuzaliwa, cheti cha kumaliza elimu ya msingi na kile cha kumaliza kidato cha nne ambapo kwa maneno yake mwenyewe alisema; \u201cJina langu halisi ni Dali Yusuph, hilo Darlington ni a.k.a yangu wakati nasoma, nadhani na wewe unafahamu kwamba unapokua, unakuwa na a.k.a. Ndiyo maana hata leo ukiingia facebook, ni mtandao wa zamani nimesajili facebook nadhani \u2018form two\u2019 nikitumia Dali Yusuph Mussa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cDali Mwasubila ni jina ambalo nilikuwa nikilitumia wakati nasoma shule ya msingi, wakati huo sijamtambua baba yangu mzazi ni nani, nadhani hiyo \u2018point\u2019 hapo umeilewa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cBaada ya kufika la saba baba yangu alijitokeza kwamba mwanangu kutokana na yote yaliyopita, mimi nilikuwa niko nje katika harakati ya kutafuta. Mawasiliano yako nilikuwa sina na hata ambao nilikuwa nikiwatuma waje kwako walikuwa hawafiki.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cKwa njia ya simu alikuja baba yangu mdogo, anaitwa Issa Zawayai ambaye yeye na baba yangu, yeye amezaliwa na mwanaume baba amezaliwa na mwanamke ndiyo kunipa simu, siku ya kwanza kusikia sauti ya mzee wangu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><\/span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/e626a-italy.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"265\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/e626a-italy.jpg?resize=400%2C265&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Sehemu ya Jiji Rome Italia<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><br \/><span style=\"font-size:large;\"><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNdiyo kuanza hapo nikakata kitambulisho changu cha uraia mpaka kitambulisho changu cha kura vyote vinasoma Dali Yusuph Musa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNa mpaka mzee kabla hajafa wakati wa uhai wake kwa sababu kuna vitu walikuwa wanasimamia watu, akaamuru kupitia \u2018power of attorney\u2019 ambayo nimeisajili enzi za uhai wake kwamba Dali mwanangu naomba usimamie vitu vyote na uviendeshe wewe ila huna ruhusa ya kuviuza ila viendeshe kama mtoto wangu wa pekee. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cAmeainisha mle na mpaka \u2018power of attorney\u2019 nimeisajili, ninayo na nililipia ardhi kwa hiyo hata \u2018copy\u2019 mkitaka na nyie kama kumbukumbu au moja ya vielelezo ninawapa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cMbeya shuleni nilikuwa natumia kama nilivyokwambia awali, nilikuwa nakaa na baba mlezi ambaye alinilea vizuri tu kama baba yangu kwa hiyo sikuweza kuona shaka yoyote kwa sababu malezi aliyonipa kama wenzangu na nilikuwa katika familia yenye furaha.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cLakini nikiwa ninasoma na kwa sababu mimi ni mtoto sijui chochote, nilitumia jina la Dali Mwasubila Simon.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cKwenye cheti sasa hapo sasa, kwenye cheti linasoma Dali Yusuph Mussa baada ya mimi kukua sasa, cheti cha darasa la saba kinasoma Dali Yusuph Mussa\u2026\u201d alisema Dali kabla ya kukatishwa na mdogo wake aliyemweleza kuwa cheti chake cha kumaliza darasa la saba kimeandikwa jina la Dali Mwasubila Simon.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Alisema alizaliwa Mkoa wa Mbeya na kuanza elimu ya msingi huko kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa amri ya baba yake aliyekuwa akiishi Italia, aliyetaka aje afahamiane na ndugu zake pamoja na kufahamu mali zake.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Dali alisema baada ya kuhamia Dar es Salaam alibadilisha jina la ubini wake na kuanza kutumia la Yusuph Musa badala la Mwasubila Simon lakini hakueleza alipokelewaje shuleni kwa jina tofauti na lile alihitimu nalo elimu ya msingi. <\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNilikuwa nikiishi kule kule, baada ya kumaliza elemu ya msingi, nilianza shule moja inaitwa Southern Highland, nilisoma pale kwa jina la Dali Yusuph Mussa kuanzia \u2018form one.\u2019<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cBaada ya hapo tena mzee akasema natakiwa nije Dar es Salaam kwa sababu nijue vitu vilipo na ndugu zangu wapo wapi kwa hiyo nikahama shule ile nikahamia Kibaha, nikahamia shule moja inaitwa Philibert Bayi, nikaanza tena upya \u2018form one\u2019 kwa sababu \u2018syllabus\u2019 za kule zilikuwa tofauti, za kiingereza ambazo wanasoma wengine lakini kufika huku nakakutana na syllabus ya Kenya kwa hiyo nikashindwa \u2018kucop\u2019 na wenzangu, ikabidi nianzae upya \u2018form one\u2019<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u2018Baadaye nikahama shule nikaenda kusoma shule moja inaitwa St George ipo Kongowe, huko ndiko nikamaliza mpaka \u2018form four,\u201d alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa maisha yake baada ya kumaliza elimu ya msingi alisema, \u201cBaada ya hapo sasa maisha yangu yakawa na vitendawili kwa sababu gani? mamlaka baba alikuwa ameshawapa watu ya kusimamia vitu umenieleawa? kulikuwa kuna magari, kulikuwa na godown, unaona ee, kulikuwa kuna nyumba, ambazo ndugu walikuwa wamejigawia wao kama wao sasa mimi wakati ule nikawa nimetengenezewa kundi la kuwa, la kuonekana ni adui kwenye familia kwa hiyo nikawa naundiwa tume tofauti tofauti.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cUkienda kwa baba mdogo anazungumza na yule mwenzie, ukienda kwa huyu anazungumza na mwenzie kwa hiyo ni mtoto ambaye nimetengezewa vikundi ambavyo havina usalama kwangu kwa sababu ni mtoto wa pekee kwanza zingatia, umeona.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cKwa hiyo sasa nikawa ni mtoto ambaye ninaishi kwa shida, baadaye nikwambia mzee, baba akapiga simu ya kufoka, moja, mbili, tano, nikamwambia hapana mzee hilo unalosema halipo mimi naomba nirudishe ulikonitoa Mbeya. Baba akagoma, akasema hapana kama maisha ya kukaa kwa watu umeshindwa basi ngoja nikutafutie nyumba, kweli akachukua jukumu la kunitafutia nyumba ambayo ilikuwa Magomeni.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><\/span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/66d67-magomeni.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"400\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/66d67-magomeni.jpg?resize=301%2C400&#038;ssl=1\" width=\"301\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Magomeni<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><br \/><span style=\"font-size:large;\"><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNa hapo wakati nimefika magomeni nimetoka likizo kukaa pale kulikuwa kuna watu tena wakiishi pale, ni watu tu baki ambao yeye nadhani walikuwa na uhusiano mzuri na mzee mmoja marehemu kwa sasa Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa anaitwa Sheikh Abilahi, ndiyo alifanya manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na mtoto wake anaitwa Mabruki.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cKwa hiyo kukatokea mzozo ambao yule akataka mimi, Mabruki ambaye alikuwa akiishi pale akataka mimi aniwekee \u2018defence\u2019 kwamba ionekana tu nitoke pale ili yeye awe huru nikamwambia mimi kule ninakokaa nataabika ndiyo maana mze amesema nije nikae hapa na hapa naomba wewe unipishe ili nipangishe ili niweze kukimu maisha yangu. Sijui unanielewa vizuri mzee wangu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cBasi kutokana na hayo nikawa ni mtu ambaye sasa nimefanikiwa, nimepata pa kuishi lakini shule tena hapo nimerudishwa ada sina uwezo wa kusoma, ndugu wana mali, nikajaribu kuwashirikisha, bwana nahitaji pesa. Mimi mwenyewe mtihani nimeende kufanya tayari nadaiwa, tayari nimefukuzwa ada. walimu tu kwa huruma kwamba huyu mtoto inabidi amalize tu mtihani,\u201d alisema Dali.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">Alipoulizwa ilikuwaje akakwama kulipa ada wakati baba yake alimtoa Mbeya na kumtafutia shule Dar es Salaam alisema; \u201cBaba yuko Italia, sasa hapo ana matatizo lakini nilikuwa sipewi taarifa kamili, wengine wananiambia anaumwa kwa hiyo nikawa ni mtu ambaye nimechanganyikiwa ambaye sina msaada.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNa wale ndugu vile ambavyo walikuwa wamevikumbatia, kwa maslahi yao wao kwa hiyo mimi nilikuwa nimetengezewa mazingira ya kuwa mtoto wa mtaani umenielewa? kuwa mtoto ambaye sisikii lakini kwa makusudi ya Mwenyezi Mungu, wao walivyopanga iwe na Mungu hakutaka iwe hivyo kwa sababu ndiyo ikawa imenisimamisha mpake leo unaniona hivi ambapo nina kampuni ambayo ninaiendesha mimi na mdogo wangu kutokana na mapito niliyopitia.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cKwa hiyo sikuwa na furaha kule, nilikokuwa kulikuwa kuna amani na furaha kwa baba mlezi siyo kwa baba mzazi. Hiyo ndiyo \u2018short story\u2019 kutokana na maisha niliyopitia baada ya kumjua mzazi wangu kwa hiyo huku kulikuwa kuna maisha magumu. Baba mlezi alinisomesha \u2018international,\u2019 shule ya gharama na bila kubaguliwa kwa chochote wala bila kuishi tofauti<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cLakini nilipokuja kwa babaangu ndiyo nikakutana na shida nyingi, chuki kwa sababu watu wengi hawakuwa na kazi za kujishughulisha, alizowea kuwasidia, kuwasomeshea watoto, kwa hiyo baada ya kuja mimi ikajengwa chuki kubwa kwa hiyo nikawa ni mtoto ambaye sitakiwi kwa sababu tu ya mali lakini mimi nilikuwa tayari kuishi na ndugu zangu wote kwa sababu ndiyo ndugu zangu nitafanyaje.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;font-size:x-large;\">\u201cNdiyo maana baba akachukua hatua ya kuniandikia ile \u2018power of attorney kwamba wewe leo mimi nipo kesho mimi sipo utataabika hao siyo watu wazuri kwa sababu mimi wakati mwingine nakubali kuongea nao maneno ili nijue mtoto wangu wanakuweka kwenye \u2018position\u2019 gani.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNdiyo akaniandikia ile \u2018power of attorney ya kwanza nikaipeleka ardhi ikadunda wakasema haijajiridhisha. Ikaja ya pili ambayo ilikuwa na picha yangu na ya kwake tukazibana ndiyo ardhi wakaipokea na penyewe bado mimi baba nikamgusia, ukisema kutangulia ni kazi ya Mungu naweza nikaanza hata mimi ukifanya hivyo unakuwa unakufuru Mungu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cLakini sikujua nini Mungu mzee wangu alimuonyesha mbele, sikujua alikiona nini mbele yake kwamba alijua anataka kufariki, sikujua kwa sababu baada ya mwezi akafariki\u2026 baba yangu alikuwa daktari, anatibu watu wakubwa tu kule, sasa kuna mtu alimtibu akafa kwa hiyo akafungwa mpaka alipokufa,\u201d alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">ITAENDELEA<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:107%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>\u00a0NA MWANDISHI WA PANORAMA SAKATA la kujipatia mali kwa njia ya ulaghai linalomuandama mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Dali Yusuph Musa sasa limeanza kuibua maswali mengi yenye utata baada ya mfanyabiashara huyo kufanya mahojiano na Tanzania PANORAMA Blog na kueleza kuwa yupo tayari kwa mapambano ambayo yatamuweka huru. Katika mahojiano hayo yaliyofanyika jana eneo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-658","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/658","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=658"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/658\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=658"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=658"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=658"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=658"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}