{"id":627,"date":"2021-05-09T16:54:00","date_gmt":"2021-05-09T16:54:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/05\/09\/moyo-wangu-usilie-tena\/"},"modified":"2022-11-10T05:26:54","modified_gmt":"2022-11-10T05:26:54","slug":"moyo-wangu-usilie-tena","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=627","title":{"rendered":"MOYO WANGU USILIE TENA"},"content":{"rendered":"<p><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">NA JOSEPH SHALUWA<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Email: <\/span><span style=\"color:#1155cc;\"><a href=\"mailto:joeshaluwa@gmail.com\" style=\"font-family:Garamond, serif;font-size:14pt;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\">joeshaluwa@gmail.com<\/a><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Simu: 0718-400146<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Facebook @Joseph Shaluwa<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Instagram @joeshaluwa<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>HANA haraka anapotembea, ukimtazama anaonekana kujiamini sana. Tabasamu mwanana linaupamba uso wake lakini mavazi yake yanaonesha asivyo mtu wa dhiki! <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Hata kama siyo sana lakini uwezo wa kubadilisha mboga ulikuwa mikononi mwake! Anatoka kwenye duka hili maalumu kwa kuuza kadi na zawadi mbalimbali lililopo ghorofa ya saba, katika Jengo la KPC Towers, katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Anatembea taratibu kuifuata lifti iliyokuwa mita chache mbele yake.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Anatabasamu! Ni kweli anatabasamu!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Tena basi alikuwa na kila sababu ya kutabasamu, maana zilibaki wiki tatu tu kabla ya ndoa yake na mpenzi wake wa siku nyingi, Joanitha.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Mkononi mwake ana bahasha ya kaki ambayo ndani yake kuna zawadi kwa ajili ya Joanitha wake. Alijua anachotakiwa kumfanyia Joanitha!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Siku zote alikuwa akinunua apple tu, mambo yanakuwa sawa! Huo ulikuwa ugonjwa mkubwa zaidi kwa Joanitha.  Alipoifikia lifti, alibonyeza kitufe mlangoni, mlango ukafunguka. Akaingia na kusimama, punde mlango ukajifunga, akabonyeza kwenye herufi G akimaanisha kwamba anataka kushuka chini.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Ni kijana mtanashati sana, anayevutia kwa kila mwanamke aliyekamilika. Anaitwa Deogratius Mgana. Mfanyakazi wa shirika moja lisilo la kiserikali jijini Dar es Salaam. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Ana furaha moyoni mwake, maana anakwenda kufunga ndoa na chaguo la moyo wake. Kwa nini asitabasamu? Hakika ana haki ya kutabasamu!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cNi kweli lazima nitabasamu, kwanza nusu ya ndoto zangu tayari zipo kwenye mstari. Lazima nijisikie vizuri,\u201d akawaza mwenyewe akiwa kwenye lifti.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Akabaki ametulia kimya akiwa amesimama kwenye lifti ile, ikaanza kushuka taratibu kwenda chini. Ghorofa ya sita, ghorofa ya tano, ghorofa ya nne&#8230;alipofika ghorofa ya tatu, lifti ikasimama. Hapo akajua kuna mtu mwingine aliyekuwa akitaka kushuka chini. Mlango ulipofunguka, wakaingia wanaume watatu, wote wamevaa miwani za jua. \u201cMambo bro?\u201d mmoja akamsalimia. \u201cPoa,\u201d akaitikia Deo. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Lifti ikaanza kushuka taratibu, walipofika ghorofa ya pili, ikasimama. Mlango ulipofunguka tu, ghafla wale vijana watatu wakamsukuma hadi nje. Mara mlango ukafunga. \u201cPaaaaaa!\u201d mlio wa risasi ukasikika. Deo akaanguka chini, akianza kuvuja damu!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">**<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Alisikia vizuri sana mlio wa simu yake lakini aliamua kupuuzia! Si kwamba hakutaka kwenda kupokea, lakini alikuwa na kazi muhimu aliyokuwa akiifanya, zaidi ya kwenda kupokea simu!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Joanitha alikuwa anapika! Chakula kizuri ambacho mpenzi wake alikuwa anakipenda sana. Alikuwa anapika viazi vya kukausha, maarufu kama maparage ambayo Deo alikuwa akipenda sana. Siku hiyo Deo alipanga kwenda nyumbani kwa kina Joanitha, Mikocheni.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Ilikuwa zimebaki wiki tatu tu ndoa yake na Deo ifungwe. Siku ambayo alikuwa akiitamani sana na kuomba ifike haraka. Mlio wa simu yake ukakatika ghafla. Akaendelea na mapishi yake jikoni lakini baada ya muda mfupi simu ikaita tena kwa mara nyingine&#8230;<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cNani huyo aaah!\u201d Joanitha akasema kwa hasira kidogo. \u201cMimi nampikia Deo wangu bwana alaaah!\u201d akatamka tena, akifunika kile chakula jikoni na kufunga kanga vizuri.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Yap! Kama ungekuwepo, ungeamini kweli Joanitha alikuwa mwanamke mrembo. Pamoja na kwamba alikuwa amevaa kanga, lakini umbo lake lenye namba nane liliweza kuonekana vyema kabisa. Joanitha alijaaliwa umbo zuri la kuvutia. Ona anavyotembea&#8230; Kama anaonea huruma ardhi!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Ana hips pana zinazozidisha uzuri wake, ana macho mazuri yenye uwezo wa kumchanganya mwanaume yeyote aliyekamilika. Labda niseme kwamba Joanitha alikuwa mwanamke mrembo sana.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Alivyofika sebuleni simu ikaacha kuita. Akachukia sana lakini akiwa anainua ili aweze kujua aliyekuwa akimpigia ili aweze kumpigia tena, akashangaa simu yake ikianza kuita tena. Kwenye kioo cha simu yake likaonekana jina \u2018My Darling\u2019. \u201cJamani, kumbe ni sweetie,\u201d akasema akipokea ili kumsikiliza.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Ilikuwa ni namba ya Deo ikionekana kwenye kioo cha simu yake&#8230;<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cYes baby, najua hujasahau kuninunulia apple na napenda kukujulisha kwamba, maparage yako yanakaribia kuiva ila sijui ungependa nikuandalie juice ya nini? Machungwa, maparachichi, maembe au mananasi? Maana kila kitu kipo kwenye friji,\u201d Joanitha akasema kwa sauti iliyojaa mahaba mazito.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Ni vile hakujua tu! Laiti angejua!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Joanitha alihisi kumkosa sana mpenzi wake Deo. Kitu pekee ambacho alihitaji kwa muda huo ni kuisikia sauti nzuri ya mpenzi wake ambayo imetulia. Hakutaka kitu kingine chochote zaidi.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Simu ilikuwa sikioni, uso ukiwa umemjaa tabasamu mwanana, akisubiri kusikia sauti ya Deo wake. Hilo tu.  Kilipita kimya cha sekunde kadhaa, kisha akasikia sauti ya upande wa pili&#8230; \u201cSamahani dada, mimi siyo mwenye simu!\u201d sauti hii ya kiume, tulivu yenye mikwaruzo kwa mbali ilisikika kwenye simu ya Joanitha. Hakuwa Deo!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cSasa kama wewe si mwenye simu, kwa nini umepiga? Kwa nini unakosa ustaarabu?\u201d Joanitha akamwuliza yule mtu akiwa na hasira. \u201cSamahani sana dada\u2019ngu, lakini nadhani ni vyema ukawa mtulivu na kuuliza kilichotokea. Si kawaida mtu kupiga simu isiyo yake kwa watu ambao wamehifadhiwa kwenye simu hiyo. Hiyo ingetosha kabisa kukufaya ugundue kwamba kuna tatizo!\u201d mtu huyo akasema akizidi kuonesha kwamba anahitaji utulivu wa Joanitha.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cNdiyo&#8230;enhee kuna nini? Hebu niambie, maana tayari nahisi nimeanza kuchanganyikiwa!\u201d<\/span><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cSina shaka wewe ndiye Joanitha!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cNdiyo!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cNi nani wako?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cNi mchumba\u2019ngu, kwani vipi?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cUsijali, tuliza moyo dada yangu. Mimi ni Dk. Palangyo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Huyu ndugu mwenye simu, ameletwa hapa na wasamaria wema, baada ya kupitishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cAnaumwa na nini dokta?\u201d Joanitha akauliza akianza kulia kwa huzuni.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cAmepigwa risasi na watu wasiojulikana katika Jengo la KPC Towers. Hata hivyo, hana hali mbaya sana, matibabu yanaendelea lakini nimeona ni vyema kukujulisha ili uwafahamishe na ndugu wengine!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cAhsante dokta kwa taarifa, baada ya nusu saa nitakuwa hapo,\u201d Joanitha akajibu akizidisha kilio chake.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Akatoka mbio hadi chumbani kwake. Hakukumbuka kwenda kuipua chakula jikoni. Akavaa haraka na kutoka hadi getini! Ghafla kumbukumbu zake zikarudi!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cMama yangu, nimeacha chakula jikoni na jiko linawaka,\u201d akawaza akirudi ndani mbio. Ilikuwa ni hatari sana, maana alikuwa anapikia jiko la umeme. Mara moja akarudi ndani na kuzima jiko, akaipua kile chakula na kutoka kwa kasi sana.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cWewe vipi mwenzetu, mbona hivyo?\u201d mama yake akamwuliza baada ya kumuona mwanaye anaonekana kuwa na haraka ambayo hakujua ni ya nini.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cNitakupigia simu mama!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cUnakwenda wapi?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cMama nitakupigia!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cJoan, mwenzako si anakuja au haji tena?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cMama Deo amepigwa risasi, yupo hospitalini,\u201d akasema Joanitha akiwa tayari ameshaingia kwenye gari.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Akapiga honi kwa nguvu, mlinzi akafungua haraka. Joanitha akaondoa gari kwa kasi sana. Alikuwa anakwenda Muhimbili, huku nyuma akiwa amemuacha mama yake mwenye mawazo sana.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Joan aliendesha gari kwa kasi sana, hakujali ajali barabarani, alikuwa tayari kwa lolote litakalotokea! Kutokea nyumbani kwao Mikocheni hadi Muhimbili, alitumia dakika ishirini!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Hakukubali kukaa kwenye foleni, aliendesha kama daladala, kwani alipenyeza pembeni, sehemu zilizokuwa na foleni kubwa. Alipofika hospitalini, akaegesha gari lake kisha akapiga simu ya Deo na kuzungumza na yule daktari.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cNimeshafika dokta!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cOk! Uko wapi?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cKwenye maegesho!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cTukutane Kibasila!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cSawa dokta.\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Bila kupoteza muda Joan akachanganya miguu hadi liilipo Jengo la Kibasila. Akiwa kwenye lango kuu la kuingilia, akamwona mwanaume mmoja mrefu aliyevaa koti jeupe na miwani, akahisi angekuwa ndiye daktari aliyekuwa akimfuata.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cSorry, ni Dk. Pallangyo?\u201d Joanitha akauliza akimkazia macho.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cYes, karibu!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cAhsante!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cNifuate!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Dk. Pallangyo akatangulia na Joanitha akimfuata nyuma. Safari yao ikaishia ofisini kwa daktari yule iliyokuwa nje ya Jengo la Kibasila. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cKaribu sana dada yangu!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cAhsante!\u201d Joanitha akajibu na kuketi kwenye kiti, kwa mtindo wa kutazamana na daktari.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cUlisema mgonjwa ni nani wako?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cMchumba wangu!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cOh! pole sana&#8230;kilichotokea ni kwamba, mwenzio amepigwa risasi ya begani, lakini inaonekana kutokana na mshtuko alioupata, umesababisha apoteze fahamu. Tunashukuru kwamba risasi haijatokeza upande wa pili, kwa hiyo tumefanikiwa kuitoa, lakini bado hajazinduka!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cMungu wangu, atapona kweli?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cUwezekano huo ni mkubwa sana lakini yafaa tuombe Mungu naamini atakuwa sawa.\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cNaweza kwenda kumuona tafadhali?\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cBila shaka!\u201d dokta akamjibu na kusimama.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Akaonesha ishara kwamba Joanitha amfuate. Akasimama na kumfuata nyuma yake.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span> <\/span><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">***<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Deogratias alikuwa amelala kimya kitandani, Joanitha akimwangalia kwa jicho la huruma, simanzi tele ikiwa imemjaa moyoni mwake. Moyo wake unashindwa kuvumilia, macho yake yanazingirwa na unyevunyevu. Chozi linadondoka!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Chozi la huzuni!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Deo ametulia kitandani, mwili wake ukiwa umefunikwa kwa shuka jeupe, isipokuwa kuanzia kifuani, bandeji inaonekana mkononi mwake. Mapigo ya moyo wake yanakwenda taratibu kabisa!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cDeo wangu&#8230;Deo&#8230;Deo jamani&#8230;amka mpenzi wangu. Naomba usife mpenzi wangu jamani. Hebu amka baby, tufunge ndoa&#8230;bado nakupenda&#8230;\u201d akasema Joanitha akilia kwa uchungu.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Deo hakusikia kitu, alikuwa katika usingizi mzito, hajui chochote kinachoendelea. Alikuwa amepoteza fahamu na hakuwa na uwezo wa kusikia chochote. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Wasiwasi wa Joanitha ulikuwa mmoja tu; kwamba Deo akifa asingeweza tena kufunga naye ndoa, tendo ambalo alikuwa akilisubiria kwa muda mrefu sana. Joanitha akazidi kulia. Alitamani sana kuliona tabasamu la Deo.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Alitaka kuona akiongea, akimbusu, akimkumbatia na kumwambia maneno matamu ambayo amekuwa akimwambia kila wakati. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>Hilo tu!<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">Lakini Deo hakuweza kufanya chochote kati ya hivyo. Alikuwa amelala kitandani kama mzigo, hana taarifa kama mpenzi wake Joanitha alikuwa kitandani mwake akilia.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span>\u201cBasi dada yangu, mwache apumzike, usijali, huna sababu ya kulia. Atapona tu!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cLakini inaniuma dokta, bado wiki tatu tufunge ndoa. Tayari ndoa imeshatangazwa mara ya kwanza kanisani, bado mara mbili ili nifunge ndoa na Deo wangu, sasa itawezekanaje tena? Si ndiyo nimeshampoteza? Si tayari nimeshapoteza ndoa?\u201d Joanitha akasema akionekana kuwa na uchungu sana.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">\u201cHapana, hana hali mbaya, wiki tatu ni nyingi sana, kabla ya muda huo atakuwa amesharejea katika hali yake ya kawaida, bila shaka atapanda madhabahuni kufunga ndoa na wewe!\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal; margin-bottom:0.0001pt; margin-bottom:0;\"><span> <\/span><span style=\"font-family:Garamond,serif; font-size:14pt;\">ITAENDELEA&#8230;<\/span><\/p>\n<p><span> <\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NA JOSEPH SHALUWA Email: joeshaluwa@gmail.com Simu: 0718-400146 Facebook @Joseph Shaluwa Instagram @joeshaluwa HANA haraka anapotembea, ukimtazama anaonekana kujiamini sana. Tabasamu mwanana linaupamba uso wake lakini mavazi yake yanaonesha asivyo mtu wa dhiki! Hata kama siyo sana lakini uwezo wa kubadilisha mboga ulikuwa mikononi mwake! Anatoka kwenye duka hili maalumu kwa kuuza kadi na zawadi mbalimbali [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3456,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[79,1],"tags":[35],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-627","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo","8":"category-uncategorized","9":"tag-mikito"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/627","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=627"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/627\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3457,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/627\/revisions\/3457"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3456"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=627"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=627"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=627"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=627"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}