{"id":6041,"date":"2024-07-19T05:04:38","date_gmt":"2024-07-19T05:04:38","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=6041"},"modified":"2024-07-19T05:21:09","modified_gmt":"2024-07-19T05:21:09","slug":"kigwangalla-abeza-bil-6-za-usajili-simba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=6041","title":{"rendered":"KIGWANGALLA ABEZA BIL. 6 ZA USAJILI SIMBA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong><em>RIPOTA PANORAMA<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">MBUNGE wa Nzega vijijini na shabiki mkubwa wa timu ya Simba amebeza usajili wa matumizi makubwa ya fedha za mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji kuwa ni ya kupaka rangi ufa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akiandika kwenye ukurasa wake wa X, zamani twitter hivi karibuni, Kigwangalla anaeleza kuwa ameona bajeti ya mwekezaji kwenye usajili wa msimu huu ya Sh. bilioni 6 na ameona masimango mengi dhidi yake kutoka kwa aliowaita mbumbumbu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika andiko lake hilo, Kingwangalla anaeleza kuwa hatachoka kutoa elimu ya bure bila kujali kama inatakiwa au haitakiwa kwa sababu hakuna elimu mbaya na hakuna ukweli ulioaibika.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNi suala la muda tu kabla haujasimama na kuthibitika. Ukweli huwa una mwendo wa kinyonga, uongo una mabawa kama tai. Kama hatujarekebisha mfumo na muundo wa timu yetu hata mwekezaji aweke nini hakutakuwa na mafanikio ya kutisha.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKuna siku mtanikumbuka. Iko hivi, hakuna alichonacho tajiri mwenye elimu akakosa, kilichofanyika ni kupaka rangi ufa&nbsp; na siyo kurekebisha ukuta,\u201d unasomeka ujumbe wa Kigwangalla.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"1024\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-1024x1024.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-6042\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-1024x1024.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-300x300.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-150x150.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-768x768.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-1536x1536.jpg 1536w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-600x600.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-696x696.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-1392x1392.jpg 1392w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-1068x1068.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-420x420.jpg 420w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO-840x840.jpg 840w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/MO.jpg 1600w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong><em>Mohammed Dewji<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Anaandika pia kuwajibu aliowaita mbumbumbu wanaomdhihaki wakimtaka asajili walau mchezaji mmoja akieleza kuwa hashindwi kusajili kwani msuli huo anao na kwamba yeye siyo masikini kwani hapo awali alichangia sana mafanikio ya timu ya Simba bila kujitangaza kwa sababu hakuwa anatafuta chochote.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLakini kwa wenye mantiki watahoji kwamba nisajili kama nani? Ili iweje? Mfumo mpya umefeli? Najiuliza, najiliuza mwekezaji kaweka bilioni 6 lini? Mchanganuo wake upo wapi? kaziweka kama kitu gani?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNajiuliza najiuliza mapato ya mwaka jana ni yepi? Anatangaza bidhaa zake kwa minaajili ipi? Yeye mwenyekiti wa bodi kwa miajili ipi? Hisa kalipa ama lah? Jibu hajalipia, anatoa wapi mamlaka na madaraka ya kuteua bodi hajalipia hisa zake? ni kwanini mbumbumbu mnafurahi? Ama kweli ni mbumbumbu?\u201d anahoji Kigwangalla kwenye ujumbe wake.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Anahitimisaha ujumbe wake kwa kuhoji zaidi kuwa ni nini kimekwamisha mabadiliko ndani ya klabu ya Simba kwa kipindi cha miaka saba sasa na matangazo ya mwekezaji yanaiingizia kiasi gani klabu ya Simba na kinatumikaje.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ujumbe huo wa Kigwangalla ambao umechangiwa na wengi kwa mitizamo tofauti umewaibua baadhi ya watu wanaodai kuwa sasa umefika muda kwa Dewji kutumia misuli yake kuanika kilichojificha nyuma ya ukoasaji wenye mwelekeo wa mashambulizi binafsi dhidi ya mwekezaji huyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA MBUNGE wa Nzega vijijini na shabiki mkubwa wa timu ya Simba amebeza usajili wa matumizi makubwa ya fedha za mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji kuwa ni ya kupaka rangi ufa. Akiandika kwenye ukurasa wake wa X, zamani twitter hivi karibuni, Kigwangalla anaeleza kuwa ameona bajeti ya mwekezaji kwenye usajili wa msimu [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":6043,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[79],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-6041","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-michezo"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/HK.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/6041","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=6041"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/6041\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":6048,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/6041\/revisions\/6048"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/6043"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=6041"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=6041"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=6041"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=6041"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}