{"id":5987,"date":"2024-07-01T11:47:41","date_gmt":"2024-07-01T11:47:41","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5987"},"modified":"2024-07-01T12:16:23","modified_gmt":"2024-07-01T12:16:23","slug":"mwarabu-adaiwa-kuua-kwa-fujo-wanyamapori-wanaolindwa-kisheria","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5987","title":{"rendered":"MWARABU ADAIWA KUUA KWA FUJO WANYAMAPORI WANAOLINDWA KISHERIA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong><em>RIPOTA PANORAMA<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PORI la Hifadhi ya Wanyamapori la Simanjiro limevamiwa na kundi la wanaodaiwa kuwa ni majangili wa kiarabu wanaowinda na kuua kwa fujo wanyamapori, wakiwemo wanaolindwa kisheria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Inadaiwa majangili hao huingia nchini kama wageni wanaokuja kumtembelea rafiki yao mwenye makazi yake hapa nchini lakini ana uraia wa Yemen na Falme za Kiarabu (UAE).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Vyanzo vya habari vilivyo karibu na mwarabu huyo anayedaiwa kujihusisha na ujangili vimeeleza kuwa anaishi mkoani Arusha na amejipenyeza kwa baadhi ya watu wenye madaraka serikalini anaotumia majina yao kujikinga na mkono wa sheria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wanyama wanaodaiwa kuuawa kwa fujo ni simba, nyumbu, ndege anayejulikana kwa jina la kori bustard na lesser bustard, digidigi na impala majike.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Inadaiwa mwarabu huyo hana leseni ya aina yoyote ya kumruhusu kufanya shughuli za uwindaji nchini lakini anafanya uharamia kwa kujificha nyuma ya wazawa wenye leseni na au vitalu vya uwindaji.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"768\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1024x768.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5991\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1024x768.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-300x225.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-768x576.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1536x1152.jpg 1536w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-2048x1536.jpg 2048w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-150x113.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-600x450.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-696x522.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1392x1044.jpg 1392w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1068x801.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1920x1440.jpg 1920w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-560x420.jpg 560w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-1120x840.jpg 1120w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-80x60.jpg 80w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-160x120.jpg 160w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG20240701134154-265x198.jpg 265w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong><em>Mmoja wa watu (mwarabu) wanaodaiwa kujihusisha na ujangili katika Pori la Hifadhi ya Wanyamapori  la Simanjiro akiwa emeshika digidigi aliyemuua kwa kumpiga risasi. (picha  zote kwa hisani ya vyanzo vya habari)<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNi mtu hatari, hana leseni lakini mbinu anayotumia kuendesha mauaji ya wanyamapori ni pesa. Anawalaghai watanzania wenye vitalu vya uwindaji na au leseni kuingia nao ubia wa kibiashara na kwa kutumia mwamvuli huo, hutekeleza vitendo vya uhalifu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLakini pia yupo karibu na baadhi ya watu wenye madaraka makubwa serikalini, anatumia majina yao kujikinga na sheria na huwa anatamba kabisa kuwa anatembea na ulinzi wa wakubwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTaarifa zake zipo kwenye mamlaka za serikali kwa muda mrefu lakini yupo, haijulikani hapa anaishi kwa kibali gani, kama mfanyabiashara au ameishapata uraia lakini yupo hapa hapa. &nbsp;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAnalo genge la majangili wenzake katika nchi za kiarabu ambao huwa wanakuja nchini kuuwa wanyama kisha wanaondoka. Na wala hawajifichi, wanatangaza kwenye mitandao biashara ya wanyama wetu wanaowaua,\u201d kimeeleza chanzo chetu cha habari.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Taarifa zaidi zinadai kuwa taasisi za serikali zenye dhamana ya kulinda wanyamapori na kusimamia sheria za uwindaji zimefikishiwa taarifa za kuwepo kwa genge hilo la maharamia takribani miaka mitatu sasa lakini zipo kimya.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jitahada za kumpata Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) kuzungumzia suala hili hazijafanikiwa, hata hivyo Tanzania PANORAMA Blog inaendelea na jitihada za kumfikia ili kupata kauli yake.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA PORI la Hifadhi ya Wanyamapori la Simanjiro limevamiwa na kundi la wanaodaiwa kuwa ni majangili wa kiarabu wanaowinda na kuua kwa fujo wanyamapori, wakiwemo wanaolindwa kisheria. Inadaiwa majangili hao huingia nchini kama wageni wanaokuja kumtembelea rafiki yao mwenye makazi yake hapa nchini lakini ana uraia wa Yemen na Falme za Kiarabu (UAE). Vyanzo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5990,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[75],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-5987","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-utalii"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/07\/IMG_20240701_134720-1-scaled.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5987","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=5987"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5987\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5998,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5987\/revisions\/5998"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/5990"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=5987"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=5987"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=5987"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=5987"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}