{"id":5655,"date":"2024-05-12T11:24:09","date_gmt":"2024-05-12T11:24:09","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5655"},"modified":"2024-05-12T11:40:58","modified_gmt":"2024-05-12T11:40:58","slug":"rumanyika-orugundu-wa-hifadhi-ya-taifa-ya-rumanyika-karagwe","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5655","title":{"rendered":"RUMANYIKA\u00a0ORUGUNDU\u00a0WA HIFADHI YA TAIFA YA RUMANYIKA \u2013 KARAGWE"},"content":{"rendered":"\n<p>RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p>RUMANYIKA&nbsp;ORUGUNDU, alikuwa Mtemi&nbsp;wa Kabila la Wanyambo aliyetawala Himaya ya Karagwe, mahali ilipo Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika \u2013 Karagwe,&nbsp;kuanzia mwaka 1855 hadi 1882.<\/p>\n\n\n\n<p>Mtemi&nbsp;Rumanyika alikuwa mtu hodari na aliheshimika sana katika jamii ya Wanyambo kutokana na uwezo wake wa kiuongozi na uhodari wake katika medani za kivita. Katika kipindi cha takribani miaka 30 ya utawala wake, aliwaongoza Wanyambo kuvuka vipindi vigumu vya njaa na kupigana vita na maadui zao.<\/p>\n\n\n\n<p>Historia inamtaja Mtemi&nbsp;Rumanyika kama kiongozi&nbsp;wa Himaya ya Karagwe&nbsp;aliyepigana na kushinda vita alizoongoza za kulinda ardhi yenye rutuba na msitu wa kiasili wa kiikweta, mahali ilipo Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika \u2013 Karagwe.<\/p>\n\n\n\n<p>Kutokana na uongozi wake mzuri na jinsi alivyowaongoza watu wake kukabiliana na nyakati ngumu, yakiwemo majanga mbalimbali, mwaka 2019, Serikali ilipoipandisha hadhi Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika \u2013 Karagwe, jina lake lilipewa heshima ya kutumika kuitambulisha hifadhi hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"768\" height=\"1024\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-768x1024.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5636\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-768x1024.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-225x300.jpg 225w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1152x1536.jpg 1152w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1536x2048.jpg 1536w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-150x200.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-300x400.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-600x800.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-696x928.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1392x1856.jpg 1392w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1068x1424.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-scaled.jpg 1920w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-315x420.jpg 315w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-630x840.jpg 630w\" sizes=\"auto, (max-width: 768px) 100vw, 768px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\"><strong><em>Mkuu wa Hifadhi ya Rumanyika &#8211; Karagwe, Kamishna Msaidizi wa Uhifadh, Charles Ngendo<\/em><\/strong>.<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p>Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Charles Ngendo ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; &nbsp;&nbsp;Karagwe,&nbsp;katika mahojiano aliyoyafanya na Tanzania PANORAMA Blog hivi karibuni kuhusu ustawi wa shughuli za utalii katika hifadhi hiyo anasema dunia bado haijatolewa tongotogo za macho ili kuweza kuona Bioanua za aina mbalimbali zilizopo Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika \u2013 Karagwe.<\/p>\n\n\n\n<p>Anaanza na historia ya eneo ilipo hifadhi hiyo akieleza kuwa, historia ya uhifadhi Tanzania imepitia vipindi tofauti,&nbsp;ikianzia enzi za utawala wa machifu uliohifadhi na kulinda maeneo yenye maumbile ya kidunia ya kipekee kwa taratibu za mila na desturi na ilipobidi hata kwa kupigana vita na maadui waliotaka kuyavamia&nbsp;maeneo hayo&nbsp;na kuyaharibu.<\/p>\n\n\n\n<p>Kamishna Msaidizi Ngendo anasema historia ya uhifadhi Tanzania inaonyesha kuwa wakati wa utawala wa kikoloni, watawala hao walitumia sheria kuhifadhi maeneo muhimu na baada ya Tanzania kupata uhuru yaliendelea kutunzwa.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika \u2013 Karagwe ni &nbsp;miongoni mwa Hifadhi za Taifa tano zilizotangazwa mwaka 2019. Ilitangazwa&nbsp;kwa tangazo la Serikali nambari 510 na&nbsp;ilianzishwa rasmi Julai 5, 2019 ikiwa karibu sana na Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cHifadhi hii ipo&nbsp;Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Kyerwa na ni miongoni mwa Hifadhi za Taifa 21 zilizo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cKabla Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe kupandisha hadhi, ilikuwa pori la akiba likisimamiwa na Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori (TAWA) na kabla ya kuwa pori la akiba,&nbsp;eneo hilo lilihifadhiwa kwa taratibu za mila na desturi&nbsp;za wenyeji ambao ni Wanyambo,\u201d anasema.<\/p>\n\n\n\n<p>Kamishna Msaidizi Ngendo anasema Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe ni ya kipekee&nbsp;ikiwa na milima yenye misitu ya Kiikweta ambayo inahifadhi bioanua za aina mbalimbali na Bonde la Kishanda lenye &nbsp;maziwa makubwa matano yanayohifadhi viumbe wa majini na kutiririsha maji yake kwenye maziwa na aridhi oevu. Maji ya maziwa hayo hutiririka hadi Mto Kagera ambao nao hutiririsha maji kwenye Ziwa Victoria.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"275\" height=\"183\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/ZIWA-VICTORIA.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5657\" style=\"width:693px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/ZIWA-VICTORIA.jpg 275w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/ZIWA-VICTORIA-150x100.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 275px) 100vw, 275px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Ziwa Victoria<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Anasema ni&nbsp;eneo lenye maumbile ya kidunia ya kipekee likiwa na milima na mabonde na mandhari nzuri zinazovutia kuangalia. Ni makazi ya aina mbalimbalia za wanyama na uoto wa asili.&nbsp;Imepambwa na maeneo ya tambarare za ukanda wa chini, miti ya aina mbalimbali na nyasi ndefu.<\/p>\n\n\n\n<p>Hifadhi hiyo ni makazi ya wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo nyati, sitatunga, nyani, chui, digidigi, mbweha, pongo, nguchiro, tumbili na wengineo.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"275\" height=\"183\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MBWEHA.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5658\" style=\"width:697px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MBWEHA.jpg 275w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MBWEHA-150x100.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 275px) 100vw, 275px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Mbweha<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"275\" height=\"183\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/NGUCHIRO.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5659\" style=\"width:697px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/NGUCHIRO.jpg 275w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/NGUCHIRO-150x100.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 275px) 100vw, 275px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Nguchiro<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Anataja pia uwepo ndege wa majini, nchi kavu na msituni ambao&nbsp;ni adimu sana duniani&nbsp;wanaopatikana kwenya hifadhi hiyo yenye maziwa ya Kabugwe,&nbsp;Kamuzinzi, Mkashambya, Mkanyasi na Mrundana ambayo hufanya eneo la hifadhi kuwa la kuvutia zaidi.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cMaziwa matano yaliyopo hifadhini yanaipa thamani kubwa kwani ndiyo ambayo tunatarajia yatatumika zaidi katika shughuli za utalii wa uvuvi&nbsp;baada ya mikakati iliyopo sasa ya kuboresha shughuli za utalii na ujenzi wa miundombinu kwenye hifadhi kukamilika.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cNi maziwa yenye mandhari nzuri kwa maana ya mwonekano wake. Maziwa yote yana mandhari ambazo zinatofautiana na pia uwepo wa maziwa hayo yanafanya wanyama waliopo kuwa na uhakika wa kupata maji misimu yote tofauti na hifadhi zilizo maeneo ambayo yana ukame,\u201d anasema Kamishna Msaidizi Ngendo.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema eneo la Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe lina misimu miwili ya mvua, wa kwanza ukianza mwezi Machi hadi Mei na msimu wa pili wa mvua huanzia mwezi Septemba hadi Disemba.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cMvua za muda mfupi za vuli huanza kunyesha Novemba hadi Disemba na mvua za muda mrefu wa masika huanza Machi hadi Mei. Maeneo haya yanapata wastani wa mvua za mililita 729 hadi 995 kwa mwaka na hali ya joto ni ya wastani wa nyuzi joto 13 hadi 26. Muda mzuri wa kutembelea hifadhi ni mwezi Januari hadi Februari na Juni hadi Agosti.<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumzia ustawi wa hifadhi hiyo katika kipindi cha miaka takriban sita sasa tangu ilipoanzishwa, Kamishna Msaidizi Ngendo anasema Serikali kupitia TANAPA imeelekeza nguvu kuimarisha miundombinu ya hifadhi ili kuifungua iweze kufikika maeneo yote hivyo kutoa nafasi nzuri kwa watalii kuitembelea.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"275\" height=\"183\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/KUJI-1.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5660\" style=\"width:697px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/KUJI-1.jpg 275w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/KUJI-1-150x100.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 275px) 100vw, 275px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Kamishna wa Uhifadhi (CC)  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Anasema TANAPA inalenga kurahisisha utalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe kwa &nbsp;kujenga barabara za ndani na nje ya hifadhi na kwamba kazi hiyo inasimamiwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Mhandisi Mshauri, Richard Matolo (Phd) na hatua&nbsp;ya sasa inayotekelezwa ni kuimarisha miundombinu ya barabara zilizopo kabla ya kuanza kujenga mpya.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cHifadhi hii bado changa. Kazi kubwa inapaswa kufanyika ili iweze kufikika pande zote na tunashukuru uboreshaji&nbsp;miundombinu ya utalii&nbsp;na hasa barabara&nbsp;za&nbsp;ndani ya hifadhi ili kurahisha utalii wa kutembea kwa miguu&nbsp;ambao umepewa kipaumbele chini ya usimamizi wa Kamishna Msaidizi Dk. Matolo. Kazi inafanyika inaonekana.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"640\" height=\"452\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5661\" style=\"width:697px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO.jpg 640w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO-300x212.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO-150x106.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO-600x424.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO-595x420.jpg 595w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO-100x70.jpg 100w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MATOLO-200x140.jpg 200w\" sizes=\"auto, (max-width: 640px) 100vw, 640px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Mhandisi Mshauri, Dk. Richard Matolo<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>\u201cSisi wasimamizi wa hifadhi hii tunasimamia maelekezo ya Kamishna wa Uhifadhi, Juma Kuji kwa umakini mkubwa. Amekuwa akisisitiza kuwa kila mhifadhi atembee chini ya unyayo wa mama (Rais Samia Suluhu Hassan) katika kazi zake ili tufikie lengo lililowekwa. Tunakwenda hivyo licha ya changamoto za kifedha zinazokwamisha baadhi ya utekelezaji wa miradi maana kama mnavyofahamu siku hizi fedha ni lazima itoke hazina, sasa zinapotokea changamoto za dharura kwa kazi yetu hii inakuwa tabu kidogo lakini tunasonga mbele,\u201d anasema.<\/p>\n\n\n\n<p>Kamishna Msaidizi Ngendo anasema katika Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe kuna maeneo matatu ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji&nbsp;wa&nbsp;kujenga hoteli na nyumba za muda.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema menejimenti&nbsp;ya hifadhi inashirikiana kwa karibu na&nbsp;TANAPA kuvutia watalii wa ndani wakiwemo wanafunzi&nbsp;ambao kwao kutembelea hifadhi hiyo ni kwenda kujifunza zaidi badala ya kutalii tu.<\/p>\n\n\n\n<p>Na ili kufanikisha hilo, anasema mikakati iliyopo sasa&nbsp;ni kuwasiliana na mawakala wa utalii (tour operator) wanaoleta watalii kwenye Hifadhi za Taifa zilizopo kaskazini&nbsp;mwa nchi&nbsp;ambako shughuli za utalii zimestawi kwa kiwango kikubwa ili&nbsp;wavutike kupeleka watalii hifadhi zilizo Kaskazini Magharibi.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema kuna mawakala wa utalii wachache katika Mji wa Bukoba wanaowahamasisha&nbsp;waanzishe utaratibu wa kuleta watalii moja kwa moja kutoka katika maeneo yaliyo jirani na hifadhi na&nbsp;kwamba&nbsp;mwitikio ni mzuri ingawa kampuni hizo bado&nbsp;changa.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia anasema hifadhi inashiriki&nbsp;maonyesho mbalimbali kwa ajili ya kuvutia wawekezaji hasa wa kitanzania&nbsp;na kutoka nje kwenda kuwekeza kwenye Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"320\" height=\"240\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5662\" style=\"width:699px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma.jpg 320w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma-300x225.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma-150x113.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma-80x60.jpg 80w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma-160x120.jpg 160w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/wanyambo-ngoma-265x198.jpg 265w\" sizes=\"auto, (max-width: 320px) 100vw, 320px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Wanyambo wakicheza ngoma ya asili ya Amakondore<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Kamishna Msaidizi Ngendo anasema Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe inafikika kutoka pande zote za nchi kwani serikali imeboresha kwa kiwango kikubwa miundombinu ya usafiri.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema mtalii anaweza kufika Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika &#8211; Karagwe kwa njia ya barabara akitokea Mji wa Bukoba hadi Omrushaka kisha anaingia eneo la &nbsp;Nyakatundu,&nbsp;yalipo makao makuu ya hifadhi.&nbsp;Barabara hiyo ina urefu wa kilometa 185.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"750\" height=\"600\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA.webp\" alt=\"\" class=\"wp-image-5663\" style=\"width:694px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA.webp 750w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA-300x240.webp 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA-150x120.webp 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA-600x480.webp 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA-696x557.webp 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/SITATUNGA-525x420.webp 525w\" sizes=\"auto, (max-width: 750px) 100vw, 750px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Sitatunga<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"1024\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-1024x1024.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5664\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-1024x1024.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-300x300.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-150x150.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-768x768.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-600x600.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-696x696.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-1068x1068.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-420x420.jpg 420w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI-840x840.jpg 840w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/DIGIDIGI.jpg 1200w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Digidigi<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Njia nyingine anayoitaja ya kufika kwenye hifadhi hiyo ni&nbsp;barabara inayopita Mji wa Kayanga hadi&nbsp;lango la Nyakatundu&nbsp;na au mtalii anaweza kupitia Uganda au Rwanda&nbsp;ambako atavuka mpaka wa kimataifa wa Kikagati\/ Murongo uliopo umbali wa kilomita nane kabla ya kuingia lango la Rugasha.<\/p>\n\n\n\n<p>Mtalii anaweza pia kutumia usafiri wa anga ambapo atatua Uwanja wa Ndege wa Bukoba kisha atasafiri kwa njia ya barabara hadi hifadhini.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA RUMANYIKA&nbsp;ORUGUNDU, alikuwa Mtemi&nbsp;wa Kabila la Wanyambo aliyetawala Himaya ya Karagwe, mahali ilipo Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika \u2013 Karagwe,&nbsp;kuanzia mwaka 1855 hadi 1882. Mtemi&nbsp;Rumanyika alikuwa mtu hodari na aliheshimika sana katika jamii ya Wanyambo kutokana na uwezo wake wa kiuongozi na uhodari wake katika medani za kivita. Katika kipindi cha takribani miaka 30 [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5656,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[75],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-5655","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-utalii"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5655","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=5655"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5655\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5666,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5655\/revisions\/5666"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/5656"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=5655"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=5655"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=5655"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=5655"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}