{"id":5632,"date":"2024-05-05T09:18:53","date_gmt":"2024-05-05T09:18:53","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5632"},"modified":"2024-05-05T09:32:39","modified_gmt":"2024-05-05T09:32:39","slug":"miguu-mitatu-hifadhini-ibanda-kyerwa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5632","title":{"rendered":"\u2018MIGUU MITATU\u2019 HIFADHINI IBANDA &#8211; KYERWA"},"content":{"rendered":"\n<p>RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p>MARA tu unapokanyaga ardhi ya Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa, miguu yako inakuwa imeelekea nchi mbili za Uganda na Rwanda na macho yako yanakuwa yanatizama mambo yote yanayoendelea ndani ya sehemu ya nchi hizo.<\/p>\n\n\n\n<p>Hili ni moja ya maajabu yaliyo kwenye hifadhi hii iliyoanzishwa rasmi Julai 5, 2019, kwa tangazo la Serikali namba 509 ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 294 baada ya kupandishwa hadhi kwa Pori la Akiba la Ibanda.<\/p>\n\n\n\n<p>Hifadhi ya Ibanda \u2013 Kyerwa ipo Kaskazini Magharibu mwa Tanzania na imepambwa na mikunjo ya milima, mabonde, tambarare, mito ya muda na ya kudumu pamoja na ardhi oevu. Ni eneo linalovutia sana.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"768\" height=\"1024\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-768x1024.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5636\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-768x1024.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-225x300.jpg 225w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1152x1536.jpg 1152w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1536x2048.jpg 1536w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-150x200.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-300x400.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-600x800.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-696x928.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1392x1856.jpg 1392w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-1068x1424.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-scaled.jpg 1920w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-315x420.jpg 315w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/IMG20240424155910-1-630x840.jpg 630w\" sizes=\"auto, (max-width: 768px) 100vw, 768px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Kaimu Mkuu wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Charles Ngendo<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Kaimu Mkuu wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Charles Ngendo amezungumzia uzuri na maajabu yaliyo kwenye hifadhi hiyo pamoja na hatua za makusudi za Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) za kutangaza hazina ya urithi wa historia ulio kwenye hifadhi hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cIbanda &#8211; Kyerwa ndiyo hifadhi pekee hapa nchini ambayo eneo lake limepakana na nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Uganda na Rwanda. Watalii wanaofika hapa wanasema ukikanyaga Hifadhi ya Ibanda &#8211; Kyerwa unakuwa umekanyaga pia Uganda na Rwanda, wameibatiza hifadhi hii kuwa hifadhi ya miguu mitatu. Ni maajabu ya Mungu yaliyo Tanzania,\u201d anasema.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema mtalii akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa anaweza kuona kwa karibu kabisa upande wa nchi ya Uganda na upande wa nchi Rwanda na hilo limekuwa likivutia watalii wengi kufika hifadhini hapo.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"300\" height=\"168\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/mto-kagera-2.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5637\" style=\"width:705px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/mto-kagera-2.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/mto-kagera-2-150x84.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 300px) 100vw, 300px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Mto Kagera<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Ngendo anasema sehemu kubwa ya mpaka wa hifadhi na nchi za Uganda na Rwanda ni eneo la maji ya Mto Kagera ambao una historia ya kipekee na kwamba watalii wengi hutumia muda wao kufuatilia historia ya mto huo wenye simulizi nzito ya vita ya Uganda na Tanzania ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda.<\/p>\n\n\n\n<p>Kama ilivyo katika baadhi ya hifadhi nyingine hapa nchini, Ngendo anasema Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa ni sehemu sahihi kwa wanafunzi kufanya ziara za kimasomo kwa sababu mbali na kujionea vivutio mbalimbali wanapata pia fursa ya kujifunza historia.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cSerikali imeweka mazingira mazuri sana kwa watalii wa ndani kuingia kwenye hifadhi, badala ya kuwaachia wageni peke yao kutoka mataifa ya mbali kuja kujifunza historia hapa, nawaarika vijana wetu na walimu wao kuja kufanya ziara za kimasoma hapa kwa sababu watapata muda wa kupumzika, kujionea vivutio vyetu na kujifunza historia, tupo tayari kuwapokea na tutawahudumia vizuri sana, hawatajuta hata kidogo,\u201d anasema Ngendo.<\/p>\n\n\n\n<p>Na hapo anaongezea kuwa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa imepakana na Hifadhi ya Akagera ya nchini Rwanda kwa upande wa Kusini Magharibi.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"620\" height=\"349\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MISITU-IBANDA.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5638\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MISITU-IBANDA.jpg 620w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MISITU-IBANDA-300x169.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MISITU-IBANDA-150x84.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MISITU-IBANDA-600x338.jpg 600w\" sizes=\"auto, (max-width: 620px) 100vw, 620px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Enel la misitu lililopo Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa.<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumzia upekee wa hifadhi hiyo, Ngendo anasema Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa imepambwa na maeneo yenye uoto wa asili kuanzia nyika za miti ya migunga, milima na mabonde, mito na tambarare zinazoifanya iwe na mandhari nzuri ya kuvutia.<\/p>\n\n\n\n<p>Anataja fursa anazoweza kupata mtalii akiwa ndani ya hifadhi hiyo \u00a0yenye nyika ya savana, milima, mito, Mto Kagera na mabonde ambavyo vimejazwa wanyama wa aina mbalimbali, mtalii anaweza kujionea wanyama wa aina ya nyati, chui, viboko, swala, nyani na kima. \u00a0<\/p>\n\n\n\n<p>Katika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda \u2013 Kyerwa, mtalii anaweza kutalii kwa gari na au anaweza kutalii kwa kutembea kwa miguu ambapo huweza kuwa karibu zaidi na wanyama na kujifunza zaidi tabia ya maisha yao ya porini.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema zipo njia mbalimbali zinazotumika kwa utalii wa kutembea kwa miguu ambapo mtalii huongozwa na askari wa hifadhi mwenye silaha kwa ajili ya kulinda usalama.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"984\" height=\"656\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5639\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park.jpg 984w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park-300x200.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park-768x512.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park-150x100.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park-600x400.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park-696x464.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Ibanda-Kyerwa-National-Park-630x420.jpg 630w\" sizes=\"auto, (max-width: 984px) 100vw, 984px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Tandala mdogo anayepatikana Hifadhi ya Taifa Ibanda &#8211; Kyerwa<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Ngendo anasema ili kufika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa, mtalii anaweza kutumia usafiri wa anga ambapo atatua Uwanja wa Ndege wa Bukoba na au anaweza kutua Uwanja wa Ndege ya Chato.<\/p>\n\n\n\n<p>Baada ya kutua, mtalii atasafiri kwa gari umbali wa kilomita 221 kutoka Bukoba mjini hadi hifadhini na akiwa anatokea Chato atasafiri kwa barabara umbali wa kilomita 441 hadi eneo la Murongo na kuingia hifadhini. Katika safari hiyo kwa njia ya barabara mtalii atajionea maeneo ya utamaduni ya kabila la wanyambo, kilimo cha migomba, mashamba makubwa ya miwa na kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"310\" height=\"163\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MIGOMBA-KARAGWE.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5641\" style=\"width:698px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MIGOMBA-KARAGWE.jpg 310w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MIGOMBA-KARAGWE-300x158.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/MIGOMBA-KARAGWE-150x79.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 310px) 100vw, 310px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Shamba la migomba linalopatikana Karagwe<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Mbali na njia hiyo, pia mtalii anaweza kufika hifadhini akitokea upande wa Uganda kupitia mpaka wa kimataifa wa Murongo au Kikagari. Baada ya kuvuka eneo la mpaka, atasafiri kwa njia ya barabara umbali wa kilomita nne hadi kuingia makao makuu ya hifadhi ambayo yapo umbali wa kilomita tatu kutoka hifadhini.<\/p>\n\n\n\n<p>Kuhusu hali ya hewa, Ngendo anasema kuna misimu miwili ya mvua; msimu wa mvua za vuli zinazoanza mwezi Oktoba hadi Novemba na msimu wa mvua za masika ambao ni wa mvua nyingi unaoanza mwezi Machi hadi Mei.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"672\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1024x672.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5640\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1024x672.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-300x197.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-768x504.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1536x1008.jpg 1536w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-2048x1344.jpg 2048w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-150x98.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-600x394.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-696x457.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1392x913.jpg 1392w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1068x701.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1920x1260.jpg 1920w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-640x420.jpg 640w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1280x840.jpg 1280w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-741x486.jpg 741w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/Angellah_Kairuki-1482x972.jpg 1482w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Ngendo anazungumzia pia upatikanaji wa huduma kwa watalii kuwa ni wa kuridhisha na hasa baada ya uongozi wa sasa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na TANAPA kuwekeza nguvu kubwa kwenye utoaji huduma bora kwa wageni.<\/p>\n\n\n\n<p>Anawataja Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki na Kamishna wa Uhifadhi, Juma Kuji kama viongozi walioingia na mwelekeo unaolenga kuimarisha huduma kwa wageni ili kuzidi kuimarisha soko la utalii kwenye hifadhi changa zenye vivutio vya kipekee.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"225\" height=\"225\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/kuji.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5642\" style=\"width:698px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/kuji.jpg 225w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/kuji-150x150.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 225px) 100vw, 225px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p><strong><em>Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Anasema msisitizo wa viongozi hao wa uboreshaji huduma kwa wageni kwenye eneo la hifadhi linalopokea mvua nyingi kwa wastani wa milimita 700 hadi 1000 kwa mwaka na wastani wa joto, ambao ni nyuzi joto 13 hadi 26, unalolifanya kuwa la ubaridi umewezesha upatikanaji huduma bora kwa wageni wanaotoka kwenye mazingira ya baridi na ya joto.<\/p>\n\n\n\n<p>Ngendo anasema pamoja na jitihada za viongozi hao kuwa na matokeo chanya, bado ipo haja kwa Serikali kuwekeza nguvu zaidi kwenye ujenzi wa hoteli na maeneo ya chakula.<\/p>\n\n\n\n<p>Anasema hivi sasa ipo hoteli moja; Ibanda Rumanyika Lodge iliyopo umbali wa kilomita tatu nje ya hifadhi yenye hadhi ya kuhudumia watalii kutoka nje ya nchi na kwa watalii wa ndani, zipo nyumba za kulala wageni maeneo ya Murongo zenye hadhi ya kati ambazo zina sifa ya kutoa huduma bora kwao.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA MARA tu unapokanyaga ardhi ya Hifadhi ya Taifa ya Ibanda &#8211; Kyerwa, miguu yako inakuwa imeelekea nchi mbili za Uganda na Rwanda na macho yako yanakuwa yanatizama mambo yote yanayoendelea ndani ya sehemu ya nchi hizo. Hili ni moja ya maajabu yaliyo kwenye hifadhi hii iliyoanzishwa rasmi Julai 5, 2019, kwa tangazo la [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5634,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[75],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-5632","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-utalii"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5632","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=5632"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5632\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5645,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5632\/revisions\/5645"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/5634"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=5632"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=5632"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=5632"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=5632"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}