{"id":5100,"date":"2023-11-21T06:43:08","date_gmt":"2023-11-21T06:43:08","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5100"},"modified":"2023-11-21T06:43:11","modified_gmt":"2023-11-21T06:43:11","slug":"ngos-16-zapaza-sauti-ukiukwaji-haki-za-binadamu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=5100","title":{"rendered":"NGOs 16 ZAPAZA SAUTI UKIUKWAJI HAKI ZA BINADAMU"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">MASHIRIKA Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs)16 yamewanyooshea kidole baadhi ya viongozi na watumishi wa serikali kwa kukiuka haki za binadamu, utawala wa sheria na katiba..<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Pia yamelalamikia kupuuzwa au kudharauliwa kwa maamuzi na amri za mahakama kunakofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa serikali.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akisoma taarifa ya mashirika hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Utetezi Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Paul Kisabo alisema yanatoa wito wa kuheshimiwa kwa amri za mahakama na yanalaani vitendo vya kudharau amri halali za mahakama.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wakili Kisabo alisema mashirika hayo yanatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi wa mahakama wanaoshiriki kuhujumu na kuwafilisi wafugaji kwa kutoa amri za kutaifisha na kuuza mali bila kufuata taratibu za kisheria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTunalaani vikali kukiukwa haki za mifugo katika Wilaya ya Ngorongoro na maeneo mengine nchini ambapo mifugo imekuwa ikikamatwa, kuuzwa au kutaifishwa kinyume cha sheria na katiba ya nchi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTunatoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwaelekeza watumishi wa serikali hasa katika maeneo lalamikiwa kuheshimu maamuzi na amri za mahakama kwani amri za mahakama zinapaswa kuheshimiwa na kila mtu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTunatoa wito kwa TANAPA na Jeshi la Polisi kuacha mara moja ukamataji wa mifugo kwenye maeneo ambayo kuna zuio la mahakama na waache kuwasumbua wafugaji kwani nao wana haki ya kumiliki mifugo kama mali halali kwa mujibu wa ibara ya 24 ya katiba ya nchi,\u201d alisema Wakili Kisabo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"768\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-1024x768.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5102\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-1024x768.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-300x225.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-768x576.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-150x113.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-600x450.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-696x522.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-560x420.jpg 560w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-80x60.jpg 80w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-160x120.jpg 160w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL-265x198.jpg 265w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/WAKILI-PAUL.jpg 1040w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong><em>Mkuu wa Idara ya Utetezi Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Paul Kisabo<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akiendelea, Wakili Kisabo alisema mashirika hayo yanalaani kitendo cha watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutesa mifugo kwa kuwanyima malisho na maji kama njia ya kuwalazimisha wamiliki kulipa faini kwa kuhofia mifugo yao kufa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Alisema mashirika hayo yanatoa wito kwa watumishi wa hifadhi za taifa kuacha tabia ya kuswaga mifugo na kuiingiza hifadhini kwa lengo la kutoza faini, kutaifisha na kuiuza na pia serikali kuchukua hatua za kisheria kwa watumishi na viongozi waliokiuka amri za mahakama.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji yaliyotokea Mbarali, kutoa taarifa kwa umma na kuchukuliwa hatua kwa wahusika kwa mujibu wa sheria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTunatoa wito wa jumla kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutekeleza maamuzi mbalimbali ya mahakama kisheria, mfano maamuzi ya mahakama za ndani, za kikanda na kimataifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"575\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-1024x575.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5103\" style=\"width:696px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-1024x575.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-300x168.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-768x431.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-150x84.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-600x337.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-696x391.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-1068x600.jpg 1068w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO-748x420.jpg 748w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/MIFUGO.jpg 1140w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong><em>Mifugo<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cMaamuzi hayo ni kama kesi ya Rebecca Gyumi, Maria Mushi, Mjomba Mjomba, kesi ya THRDC, LHRC na MCT iliyoamriwa na Mahakama ya Afrika Mashariki mwaka 2019, THRDC na LHRC iliyoamriwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kesi ya Mchungaji Mtikila, kesi ya Jebra Kambole na kesi ya Bob Wangwe ya wakurugenzi wa uchaguzi zilizoamriwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na nyingine nyingi,\u201d alisema Wakili Kisabo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali yaliyotoa tamko hilo ni Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), &nbsp;Baraza la Wanawake Wafugaji (PWC), &nbsp;Shirika la Uraia na Msaada wa Kisheria (CILAO), Mtandao wa Mashirika ya Kifugaji (PINGOs Forum), Ujamaa Community Resource Team (UCRT) na Shirika la Kukuza Haki za Binadamu (OPH).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mengine ni Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Shirika la Uhifadhi wa Mifumo ya Asili na Jadi (TEST), Shirika la Maendeleo Jumuishi wilayani Ngorongoro (IDINGO), Jukwaa la Ardhi Tanzania, Shirika la Kuinua na Kusaidia Maisha ya Wafugaji (PALISEP), Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Green Planet Initiative (GPI) na Pan African Lawyers Union (PALU).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA MASHIRIKA Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs)16 yamewanyooshea kidole baadhi ya viongozi na watumishi wa serikali kwa kukiuka haki za binadamu, utawala wa sheria na katiba.. Pia yamelalamikia kupuuzwa au kudharauliwa kwa maamuzi na amri za mahakama kunakofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa serikali. Akisoma taarifa ya mashirika hayo mbele ya waandishi wa [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5101,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-5100","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/11\/KATIBA.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5100","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=5100"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5100\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5104,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/5100\/revisions\/5104"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/5101"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=5100"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=5100"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=5100"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=5100"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}