{"id":4672,"date":"2023-06-06T07:39:33","date_gmt":"2023-06-06T07:39:33","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=4672"},"modified":"2023-06-06T07:39:35","modified_gmt":"2023-06-06T07:39:35","slug":"skandali-ya-acisp-kutinga-bungeni","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=4672","title":{"rendered":"SKANDALI YA ACISP KUTINGA BUNGENI"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">SAKATA la Chuo Kikuu cha Bima na Mifuko ya Jamii Afrika (ACISP) kutumia mgongo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) kunufaika kifedha linatarajiwa kuibuliwa bungeni kabla ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wakizungumza na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu nia ya kuliibua sakata hilo, baadhi ya wabunge wanaokusudia kulibeba, wamesema lengo ni kukinusuru na anguko linalokinyemelea, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kinachomilikiwa na Serikali.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wabunge hao waliozungumza kwa sharti la kuhifadhiwa majina yao kwa kile walichodai kulinda dhamira yao njema ya kukinusuru IFM isikwamishwe na wanufaika wa jambo hilo, wamesema kuanzishwa kwa ACISP kama mshindani wa IFM huku kukiwepo tuhuma za kukihujumu chuo hicho cha Serikali ili kukipa nafasi ACISP kuteka soko la utoaji huduma ya elimu ya Bima ni jambo lisilokubalika.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha wamesema, madai kuwa TIRA imekuwa ikitumia misuli yake kama taasisi ya Serikali kukusanya na ama kuchangisha fedha kutoka kwenye taasisi mbalimbali za Serikali zinazokwenda kuinufaisha ACISP ni jambo linalopaswa kuchunguzwa ili ukweli ufahamike.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSisi wabunge kazi yetu, pamoja na mambo mengine ni kuishauri Serikali. Sasa katika hili wala siyo kwamba tunakwenda kuumana na mtu maana kuna mambo yapo wazi kabisa kwenye hili, Serikali ifanyie kazi tuhuma zilizopo ili kuondoa dosari zote na hatua zichukuliwe panapostahili.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHizi taasisi za Serikali zinazoandikiwa na TIRA kutoa fedha halafu zinapelekwe kwenye hicho chuo cha binafsi iwe moja kwa moja au kwa njia za panya zinafahamika. Huyo anayeandika barua hizo na taasisi ya Serikali anayoitumia kuandika kwa ajili ya michango ya fedha zinazokwenda kwenye chuo hicho anafahamika, Uchunguzi ukifanyika kila kitu kitakuwa wazi na hicho ndicho tunataka kwenda kuishauri Serikali, ifanye uchunguzi na ripoti ya uchunguzi iwekwe wazi.\u201d alisema.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Haya yanajiri baada ya Kamishna Mkuu wa TIRA, Abdallah Baghayo Saqware kuanzisha ACISP. Uanzishwa wa chuo hicho ambacho ni mshindani wa IFM kuliwainua wadau wa bima nchini waliotuhumu hatua hiyo ya Saqware kuwa ni ukiukwaji wa maadili katika utendaji wa soko la Bima linalodaiwa kuporomoka kwa kasi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Inadawa ACISP sasa kinatangazwa kuwa chuo bora zaidi katika ukanda wa Afrika wa Mashariki kinachofundisha masomo ya Bima na kwamba kumekuwa na jitihada za makusudi za kuihujumu IFM ili kudhoofisha ubora wake wa utoaji elimu ya Bima, lengo likiwa kukiinua ACISP.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha inadaiwa, Saqware amekuwa akitumia wadhfa wake katika TIRA, taasisi ya Serikali ambayo yeye ni kiongozi wake mkuu<a> kualika taasisi mbalimbali za Serikali kushiriki shughuli za ACISP kwa kuchangia fedha na ili kuficha uhalisia wa makusanyo hayo ya fedha na kujenga ushawishi kwa taasisi za Serikali kushiriki shughuli za chuo hicho na kukichangia, amekuwa akiwaalika viongozi wazito serikalini wakiwemo mawaziri na wakati mwingine hata Waziri Mkuu kuwa wageni rasmi.<\/a><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Saqware ametafutwa na Tanzania PANORAMA kuzungumzia hilo na kueleza yupo safarini mkoani Dodoma. &nbsp;&nbsp;<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA SAKATA la Chuo Kikuu cha Bima na Mifuko ya Jamii Afrika (ACISP) kutumia mgongo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) kunufaika kifedha linatarajiwa kuibuliwa bungeni kabla ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti. Wakizungumza na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu nia ya kuliibua sakata hilo, baadhi ya wabunge wanaokusudia kulibeba, wamesema lengo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":4673,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-4672","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/06\/tira-pics.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4672","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4672"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4672\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4674,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4672\/revisions\/4674"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/4673"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4672"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4672"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4672"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=4672"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}